Ukipenda kile unachofanya, hutahisi kana kwamba ni kazi kamwe
Jamii wakati mwingine hutufundisha kutafuta zile kazi zenye mshahara mkubwa kama njia ya kuyafikia mafanikio, lakini pesa haziwezi kukunulia furaha.
Wakati mwingine kutafuta kile unachopenda kufanya zaidi duniani, na kuwa na bahati ya kujipatia pesa kwa kukifanya, ndio ufunguo wa furaha.
Wakati Mwandishi mmoja wa Nijeria aitwaye Chimamanda Ngozi Adichie alipokuwa msichana mchanga, watu walisema kwamba alifaa kuwa daktari. Hata alienda chuoni kusomea taaluma ya famasia. Lakini moyo wake ulikuwa na mipango mingine. Chimamanda alikuwa anapenda kusoma vitabu tangu akiwa mtoto na alijua kwamba alipenda kuandika, kwa hiyo akaacha sayansi na kuanza kuandika kwa ubunifu wakati alipopata ufadhili wa kusoma huko Marekani. Hii ilimfanya akaandika kitabu cha riwaya kilichoshinda tuzo wakati alipokuwa katika mwaka wake wa mwisho chuoni. Huenda wengi walidhani ingekuwa vizuri zaidi kama angekuwa mwanafamasia, lakini hakuruhusu hayo yamfanye aache kuifuata ndogo yake!
Je, unapenda kupika au kuoka? Je, unapenda sanaa? Je, marafiki zako na familia yako hukuomba uwasaidie katika hisabati kwa sababu wewe ni mzuri sana kwazo? Vizuri sana, huenda umepata taaluma yako ya usoni! Kufanya kitu unachopenda kabisa kutakufanya uhisi kana kwamba hufanyi kazi kamwe.
Huhitaji wakati wote kuwa na bidhaa nyingi au pesa ndipo uanze biashara. Anza pole pole na, kadri unavyofanya kazi kwa bidii na upate mafanikio madogo, mambo yatakua. Unaweza kuanzia nyumbani, na unaweza kuwahusisha marafiki na familia yako katika miradi yako.
Kuwa makini shuleni, ongea na watu walio na kazi zile unazopenda. Fanya utafiti wako na uchague njia ya elimu inayokufaa. Kwa mfano, kazi nyingine zahitaji shahada au cheti maalum. Lakini kwa kazi nyingi, elimu ya sekondari inatosha, na hata ikiwa umeshindwa kumaliza shule – inawezekana kutumia talanta au ujuzi wako kujipatia pesa. Kufanya vizuri shuleni katika kiwango chochote kile kunaweza kusaidia kufungua milango ya kutimiza ndoto zako baadaye, hata ikiwa hujui ndoto hiyo ni gani.
Kila mtu anataka kujipatia kipato cha kukimu maisha na kila mtu anataka kuishi maisha mazuri. Pesa ni nini ikiwa unachukia kazi unayofanya kila siku? Bado ni kijana na una muda wa kutambua kile unachopenda zaidi, kwa hiyo usiwe na wasiwasi ikiwa bado huna hakika. Tumia wakati huu kuchagua kati ya yale yaliyoko!
Share your feedback