Pata uzoefu katika kazi unayotaka
Enyi Springsters
Sisi sote tuna ndoto na matarajio ya kile tunachotaka kufikia katika maisha, lakini ni rahisi kujisikia kutishika na kuchanganyikiwa kuhusu wapi utakapoanzia. Usiogope… Hakuna haja ya kujiskia kuzidiwa na hofu! Kitu cha msingi ni kuanza kidogo kidogo.
Hatua kubwa ya kwanza ni kupata kivuli cha kazi. Hii ni pale ambapo unaenda kazini na mtu ili uweze kuona kinachohusu kazi yao. Ni njia nzuri ya kukusaidia kuamua unataka kuwa nini katika siku zijazo. Na ikiwa kuna kazi inayokuvutia unaweza kupima ikiwa ni hiyo unayotaka!
Kuanza: Tafuta kampuni au shirika linalofanya kazi katika sekta ya viwanda ambayo unavutiwa nayo. Unaweza kuuliza idara ya uajiri, na kuelezea kuwa unatafuta ajira ya kukuza uzoefu. Kwa kawaida, hii itakuwa kwa siku au wiki. Sheria ya kwanza? Daima kuwa salama. Uliza mtu mzima kukusaidia kutafuta shirika na kujihakikishi kwamba ni la kweli, na kwamba hutakuwa hatarini.
Kuwa msaada: Wajua ni kitu gani ambacho kila mtu hupenda? Watu ambao ni msaada. Jitambulishe kwa watu walio karibu nawe, waulize wanachofanya, waambie kwanini uko pale na toa msaadai wakati wowote unapohitajika. Tunapotia bidii, watu huonyesha shukrani yao.
Uliza tu: Hakuna kitu kama swali la kijinga! Mojawapo ya faida ya ajira ya kukuza uzoefu ni kwamba unapata kukutana na watu ambo wana majibu ya maswali yako, na huenda wakakupa taarifa zingine muhimu ambazo hukujua kama unazihitaji.
Tenda sehemu yako: Kuwa mtaalamu. Kumbuka kuwa kila fursa tunayopata kukaribia ndoto zetu ni ya muhimu. Kwa hivo tumia kikamilifu milango inayofunguliwa kwa ajili yako. Fika mapema, usijibu simu yako katika mkutano au wakati wa kazi.
Kujaribu mambo kwa kiwango kidogo kutakupa ujasiri zaidi wa kuchukua hatua katika kutimiza ndoto zako.
Kila la kheri Springster, kuwa na ujasiri na ujiamini
Share your feedback