Nitawezaje kupata kazi?
Rafiki wangu wa dhati Abbie huwa na kazi nyingi kila wikiendi katika duka la mtaa la matunda. Kaka yangu hufanya kazi na kumaliza kazi ya upelekaji usiku sana kila siku. Lina humsaidia mama yake kwenye saluni yake ya wanawake, kufagia nywele na wakati mwingine huruhusiwa kusaidia kuosha nywele za wateja.
Nilituma wasifu wangu kwenye migahawa yote mtaani na maduka, na bado sikupata kazi. Sikuweza kufanikiwa kupata nilichokitafuta sababu sikuwa na uzoefu wa kutosha.
Ninapenda mavazi, lakini wasichana wote ambao walifanya kazi katika maduka ya nguo walikuwa wakubwa kidogo na walikuwa na uzoefu wa mauzo. Hakuna mtu ambaye angenipa nafasi!
Kwa kuwa marafiki zangu walikuwa wamebanwa na kazi, niliamua kufanya jambo la maana. Nilisoma jinsi ya kushona, kutia rangi na kutengeneza nguo. Nilikodisha vitabu kutoka kwenye maktaba na kuchunguza vidio mtandaoni, pamoja na ujuzi wangu kutoka shuleni. Kwa njia hii, likizo ijayo, nitakuwa na uzoefu zaidi wa kupata kazi.
Kwa fedha zangu za mfukoni, nilienda madukani kununua vipande vya nguo nilivyofikiri naweza kufanyia kazi. Nilitengeneza vipande kadhaa na kuvivaa kwenda shuleni. Nilipata pongezi nyingi – “Ulipata wapi skati hiyo?” “Mkoba huo ni mzuri!” “Ninapenda viatu vyako!”
Wikiendi hiyo nilienda kwenye soko la mtaa na kuuliza baadhi ya wamiliki wa maduka jinsi yalivyofanya kazi na ni kiasi gani ningehitaji kuuza ili kupata faida. Nilimuomba mama anisaidie kulipa kodi ya duka, nami ningemlipa kwa fedha zangu za mfuko, au kwa faida yangu.
Punde nilikuwa napata faida ya kutosha kukodisha duka kila mwezi bila msaada wa mama yangu.
Mwanzoni, nilihisi sina tumaini wakati hakuna mtu angenipa fursa. Lakini badala ya kusubiri na kutumai mtu aniajiri, niligeuza shauku yangu kuwa malipo!
Share your feedback