Je, unapaswa kuwa?

Mtu ambaye ndio mfano wako wa kuiga ako aje? Acha tujue!

Maisha yanaweza kuwa magumu! Kuna ushawishi na maoni mengi sana yanayokuzunguka, kutoka kwa marafiki na wafanyakazi wenza hadi walimu, wazazi na ndugu, bila kutaja mitandao ya kijamii, huwa ni vigumu kujua ni nani utakayesikiliza na maamuzi ambayo ni mazuri au mabaya.

Sisi wote tuna watu wazuri wa kuiga. Pengine kwako ni msichana mkubwa anayeishi hapo chini barabarani na amefanikiwa kuendesha biashara yake ndogo kutoka nyumbani; au mwalimu wako anayetambua uwezo wako na anakusukuma ufanye mambo makubwa; huenda ikawa shangazi na mjomba wako ambao wana hekima na ujasiri mwingi; au pengine ni msichana anayekuhimiza kwenye Instagram ambaye anafanya mambo yake. Lakini, watu wa kuiga wanaweza kuwa washauri wazuri?

Unawezaje kujua ikiwa unaweza kuamini mtu huyo kukupa mawaidha na ushauri, na kukusaidia kufanya maamuzi bora?

Anza na hatua hizi rahisi:

1. Tengeneza orodha

Andika maadili yako, kwa nini unahitaji mshauri na nini unachokitafuta katika mshauri. Hii itakupa dhana wazi ya haswa unachokitaka.

2. Anzisha mazungumzo

Ikiwa unahisi salama kufanya hivyo, zungumza na watu wako unaowaiga mfano wao. Waulize wanachokifikiria humfanya mtu kuwa mshauri mzuri, kama wanahisi wanaweza kuwa mmoja, na kama wanafikiria kuna faida za kuwa mmoja. Andika majibu yao ili uweze kulinganisha mawazo ya kila mtu na uamue ni nani unayekubaliana na yeye zaidi. Maoni ya kila mtu yanapaswa kukusaidia kujua ni nani unayehisi anaweza kuwa mshauri mkuu. Hakuna mmoja wao anaweza kuwa anayefaa, lakini mtu ambaye wanamjua anaweza kuwa anayefaa! Sasa, unaweza kuwauliza?

3. Chukua hatua

Ikiwa ni mtu unayemjua, omba dakika tano za muda wake ili mzungumze. Kisha kuwa mwaminifu– waeleze utashukuru kupata msaada na ushauri katika maisha yako, na kwamba unahitaji kujua kama unaweza kuwaamini kuweka siri zako na hao wakupe ushauri bila kukuhukumu. Asilimia tisini na tisa watahisi vizuri na watakuwa tayari kukusaidia. Ikiwa ni mtu ambaye amependekezwa kupitia rafiki, tafadhali omba rafiki yako akutambulishe kwake kupitia barua pepe, simu au uso kwa uso. Kumbuka, ikiwa unakutana na mtu kumbuka kuwa na mtu mwingine na wewe na umfahamishe mtu mzima unayemwamini uko wapi na uwe na muda wa kutosha wa maongezi kwenye simu yako ili upige simu iwapo kuna tatizo.

Si ni vizuri sana kuwa na watu wengi wa kuiga, ambao wanaweza kuwa washauri wakuu pia? Mshauri anayefaa yuko mahali nje akikusubiri!

Share your feedback