Kuwa bosi wewe mwenyewe

...anzisha biashara ndogo

Girlboss ni moja ya heshitegi ninazopenda sana katika mitandao ya kijamii. Inawaenzi wasichana wadogo na wakubwa wanaofikiria na kutenda kama mabosi. Hawa ni wasichana wadogo kama sisi. Baadhi yao wamepitia mwanzo mgumu katika maisha na wamekumbana na changamoto nyingi. Hao ni mabosi kwa sababu waliamini mawazo yao ya biashara, na kuyatekeleza.

Kama Mbali. Hata ingawa yeye ana miaka 15, yeye ni mkulima wa mjini, na anauza mboga. Au Amina (11) na Kemo (13) - kampuni zao zinauza bangili za ushanga.

Wamenihamasisha kuanzisha biashara ndogo. Nilimwomba dada yangu anisaidie. Anasema lazima nianze na wazo, na kisha niangalie katika jamii yetu nione ikiwa kuna huduma au bidhaa ninayoweza kuuza. Nina kompyuta ndogo na babangu huniruhusu kutumia data yake kuingia mtandaoni. Kwa sababu watu wengi katika eneo langu wanatafuta kazi, nitaanza kuandika wasifu wangu wa kikazi vizuri.

Pia ninahitaji mpango wa biashara. Hii inamaanisha kuwa na stakabadhi inayoeleza jinsi biashara yangu itakavyoendeshwa, na malengo niliyo nayo juu ya biashara yangu.

Kisha kinachofuata ni ushauri. Hili ni muhimu sana! Mshauri ni mtu anayetumia ujuzi wake kukufundisha na kukusaidia wewe. Mtu huyu anaweza kuwa mfanya biashara aliyefanikiwa katika jamii yako. Pia unaweza kujaribu kutafuta msaada kutoka kwa mashirika yanayosaidia wafanya biashara vijana. Pia wanasaidia katika ufadhili wa kipesa.

Kwa hiyo si unaona jinsi ilivyo rahisi sana kutimiza ndoto zako. Anza na wazo, kisha andaa mpango wa biashara, tafuta mshauri, changisha pesa na kisha songa mbele!

Share your feedback