Jinsi ya kuhoji kama MKUBWA

Ushauri ambao si wa siri kutoka kwa mtu anayejua

Hujambo! Jina langu ni Shanti, na nina miaka 24. Jambo ambalo linanifanya kuwa mzee zaidi. Lakini hilo pia linamaanisha kuwa ninajua mambo mengi. Mambo muhimu! Mambo ya watu wazima. Na mambo ninayojua... yatakupa kazi unayotaka siku moja.

Kwa sababu ya kazi yangu? Ninawahoji watu wanaotaka kazi kwenye kampuni ninayofanya kazi. Kumaanisha siku nzima ninahitajika kufanya maamuzi magumu sana kuhusu anayechaguliwa na asiyechaguliwa. Kuna MENGI ya kuzungumzia, kwa hivyo tufanye hivi!

Mambo Muhimu Kwanza
Kuitwa kwenye mahojiano kunamaanisha mambo mawili mazuri. Kwanza, kunaamisha uliwasilisha CV yako — safi! — kumaanisha ulichukua jukumu la maisha yako. Pili, mtu aliona CV yako na kuamua kuwa alitaka kuzungumza nawe. Tayari unaendelea vizuri.

Kabla ya Mahojiano
Salale! Usiwe na wasiwasi. Ukiwa na wasiwasi, hujitambui. Sababu kubwa ya mtu kama mimi kutaka kuzungumza nawe ni kuwa tunafikiria kwamba huenda ukafanya kazi nzuri.

Njia bora ya kutokuwa na wasiwasi? Fahamu mambo yako.

Tafuta taarifa kuhusu kampuni unayotaka kufanyia kazi na kazi unayotaka. Tafuta kwenye intaneti ili ujue ukweli wako wote na uweze kuuliza maswali mazuri. Hakuna kitu kizuri kama kumhoji msichana ambaye amejiandaa kuzungumzia masuala ya biashara.

Vaa Kwa Ajili ya Kazi Unayotaka
Kila kazi ina matarajio tofauti ya kile unachopaswa kuvaa kazini. Katika kampuni nyingine, unapaswa kuvaa sare kila siku. Nyingine, unaweza kuwa na uhuru zaidi wa kujieleza. Dada yangu huvaa dangrizi kazini kwake kila siku. Ningefanya hivyo kazini kwangu, ningekuwa taabani.

Chukua kitu kinachofaa kitakachokufanya uhisi jasiri na mtaalamu na zaidi ya yote, kawaida. Kuvaa nguo za kawaida kupita kiasi ni kukosa heshima — wakati fulani mtu alihojiwa akiwa amevaa ndara na nusra nizirai — lakini usivae nguo kupita kiasi. Ikiwa hujui kabisa, mwulize mama yako, shangazi yako, dada yako mkubwa... mtu yeyote unayefikiria atakupa ushauri mzuri.

Ikiwa umezoea kujipodoa, jipodoe. Ikiwa hujazoea usifanye hivyo. Haijalishi.

Mfanyabiashara wa Kike Anayevutia na Jasiri
Kwa hivyo, umefika hapa. Inaweza kuwa afisi, au mkahawa. Labda kuna watu wengi wenye shughuli wanaoenda hapa na pale. Labda umekaa kwenye kiti ukumbini, ukisubiri kuzungumza. Hapa ndipo unapopata wasiwasi, sivyo?

Usiwe Na Wasiwasi. Hata ukiwa nao, jaribu kutafuta ujasiri ndani yako na uwe nao. Ikiwa una wasiwasi, unabadilika na kuwa si wewe. Wanataka kukuajiri wewe.

Hivyo, sasa ni wakati wa kuzungumza. Salamu yako ya mkono ni muhimu sana. Kutabasamu ni muhimu. Mkazo wa macho ni muhimu. Dumisha pumzi yako, zungumza polepole na kwa ujasiri. Kaa mbele kwenye kiti chako, na usikilize kwa makini zaidi kile kinachosemwa.

Mhojaji anapokamilisha maswali na ufafanuzi, huu ni wakati wako kuuliza maswali.

Kitu cha kuuliza?

Sawa, unaweza kuuliza chochote kinachohusu kazi hiyo. Ikiwa uliufanya utafiti wako awali, huenda tayari una maswali yanayofaa. Maswali hayakosi heshima — yanakuonyesha kuwa wewe ni mtafakari mzuri, si roboti inayosema tu ndiyo kwa kila kitu.

Jambo la Mwisho
Kumbuka: njia pekee ya kuanguka ni kuacha kufanya jambo! Ukiwa na mahojiano mabaya — nimekuwa nayo takribani sita! — jifunze kutokana na makosa yako na ufanye vyema wakati mwingine.

Sasa nenda na ujitahidi, msichana!

Share your feedback