Jinsi msichana mmoja alivyopata tumaini na usaidizi.
ina langu ni Bharti na nililelewa katika kijiji kidogo kule kaskazini mwa India. Kuna familia 40 pekee katika kijiji chetu na wengi wetu hatukuwahi kupata fursa ya kuenda shuleni, hata shule ya binafsi. Wazazi wangu wangeweza tu kumpeleka mtoto mmoja kwenye shule ya binafsi na licha ya ukweli kuwa nilikuwa mwerevu kati ya ndugu zangu wote, ni kaka yangu mkubwa ambaye alichaguliwa. Nilijaribu kujadiliana na wazazi wangu lakini majadiliano hayakufaulu. Kwanza, nilikasirika sana na hivyo kuacha kutia bidii shuleni ili kuasi familia yangu.
Ulikuwa wakati huu ambapo Nivi Madam alikuwa mwalimu wangu katika Darasa la 6. Nivi Madam alikuwa mwalimu wangu wa hisabati katika Darasa la 5 na alipoona alama zangu zikipungua, aliniita na kuniuliza kilichokuwa kibaya. Nilimweleza fursa niliyokuwa nikipoteza kwa sababu wazazi wangu walikataa kubadilisha namna walivyokuwa wakifikiria. Kisha akaniongoza kwa kuchukua hasira zangu na kuzigeuza kuwa kitu kizuri. Aliniambia nisiangazie mawazo na hisia mbaya nilizokuwa nikipitia bali kutumia ujuzi na vipaji vyangu kutia bidii hata zaidi. Alisema, unapotia bidii, una uhakikawa kupata tuzo.
Nivi Madam alinihimza kumthibitishia kila mmoja kuwa nilikuwa na uwezo. Kwa kutosoma, kulikuwa kuwathibitishia kwamba walifanya uamuzi bora. Mwishoni mwa Darasa la 6, aliniambia kuhusu ufadhili mchache wa masomo uliokuwa ukipewa wanafunzi wanaofanya vyema kwenye mitihani yao. Wanafunzi hawa wangepata fursa ya kuenda kwenye shule ya binafsi na hata sare na vitabu vyao vingelipiwa! Hii ilikuwa ndoto yangu na nikaamua kutia bidii zaidi ili kufanya vyema kwenye mitihani yangu. Wazazi wangu walinisaidia sana na matokeo yalipotokea, nilifanya vyema zaidi na kuweza kupata ufadhili wa masomo.
Leo hii ninaenda kwenye shule ya binafsi ambayo iko umbali wa saa nne kutoka nyumbani. Kwa sababu ya umbali, nilipewa fursa ya kukaa kwenye hosteli ya shuleni. Nimepata marafiki wengi na nina ndoto ya kuwa daktari siku moja na kuwasaidia watu wengine. Ikiwa Nivi Madam asingalinisaidia kugeuza hasira zangu kuwa kitu kizuri – nisingalikuwa hapa!
Kumbuka: Hadithi imehamasishwa na tukio la hali halisi ya maisha ya Tech for India Mentor.
Share your feedback