Ni mimi! Mvunjaji wa mnyororo wa wa mzaha!

Wapendwa watu wa mizaha, nina habari mbaya kwenu! Sisi, Springsters!

Kwa wengi wetu, ni kawaida sana kuwa huwa tunatazama taarifa na habari zilizowekwa katika vikundi vyetu vya gumzo na kwenye mitandao yetu ya kijamii. Wazazi wetu wengi hupenda kushiriki. Jamaa wetu wengi hupenda kushiriki. Marafiki wetu wengi hupenda kushiriki. Sisi wakati mwingine hupenda kushiriki pia!

Hivi majuzi, vikundi vyetu vya gumzo na milisho ya mitandao ya kijamii imejaa makala, hasa kuhusu COVID-19, janga, karantini, na habari za afya.

Wakati mwingine, taarifa hizi ni muhimu na za kusaidia. Wakati mwingine? Pia tunafahamu kuwa taarifa hizi zilizoshirikiwa na familia na marafiki wetu haziwi za kweli asilimia 100.

Na wakati ambapo sio za kweli, huitwa mzaha. Na inawezakuwa vigumu kuzitambua! Jumbe za mzaha huundwa tu ili kusababisha kuchanganyikiwa na taharuki, na huwa hatari sana kwa kuwa husikika kama ambazo zinawezakuwa za kweli.

Na sehemu mbaya zaidi? Mizaha hii inaweza kuwa inashirikiwa na watu unaowapenda katika familia yako. Hawajui wanafanya hivyo, wanajaribu tu kusaidia. Lakini kwa kuwa ujumbe unaonekana kuwa kama wa kweli na unatoka kwa mtu wa familia, ni rahisi kuona jinsi ambavyo ujumbe usiofaa unaweza kuenea kama mnyororo kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Hivi karibuni, hakutakuwa na anayefahamu ni yapi ya kweli na ni yapi ambayo ni uongo. Katika dharura, hiyo ni hatari sana! Tunachohitaji sasa ni watu ambao watauvunja mnyororo usiendelee kuenea.

Fuata hatua hizi na uwe Mtu wa Kuvunja Mnyororo wa Mzaha!

  • Chunguza tena iwapo taarifa hizi hakika ni za mzaha. Unaweza kufanya hivi kwa kuchunguza chanzo cha taarifa hizi. Iwapo sio taarifa jukwaa halali ya taarifa ambayo unaweza kuiamini, huenda ikawa ni mzaha.

  • Jiepushe na kutoa maoni na kutoa majibu kuhusu taarifa hizi! Mara tunapotambua kuwa ni mzaha, hatupaswi kuchangia kufaulu kwa mzaha huu kwa kuushiriki au kutoa maoni. Jinsi chapisho linavyosomwa au kutazamwa na wengi, ndivyo huwa hatari.

  • Ripoti kwa kutumia kipengele cha jukwaa. Mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter na Instagram kwa kawaida huwa na kipengele ambapo unaweza kuripoti maudhui. Kitumie na uwaombe kuuondoa mzaha huu.

  • Iwapo umeshirikiwa na marafiki au watu wa familia katika kikundi cha gumzo, jaribu uwapinge kwa upole kwa kutumia ukweli na uwaambie waache kushiriki uoga kwa kuwa hilo ndilo hakika wazambazaji mzaha hutaka kufanya! Hata tuliuandika mwongozo wa kukusaidia kuzungumza na jamaa waliotuzidi kwa umri.

Sio rahisi kupambana na hali ya COVID-19, hasa wakati ambapo mizaha inasababisha hali ya kuogofya na hata kushtua zaidi kwa watu unaowajali. Fanya uwezavyo kutamatisha uvumi na upigane na uongo kwa ukweli: pata habari, kuwa mwangalifu, na uwe mtu wa kuvunja mnyororo ambaye anaifanya jamii yake kuwa salama!

Kaa salama, Springsters!

Share your feedback