Njia Tatu za Kuwa Pamoja Mnapokuwa Mbali

Shughuli za mbali bado zinaweza kuwa za kuburudisha kama zile za kutoka nje za IRL!

Kuna janga linaloendelea! Kwa wengi wetu, hii inamaanisha kuwa lazima tukae nyumbani — na kusalia nyumbani kunaweza kuifanya hali ambayo tayari ni ya kufadhaisha kuwa mbaya zaidi. Ni sawa kuhisi hivi — na hauko peke yako, kwa kuwa wasichana ulimwenguni kote wanahisi hivyo pia!

Njia moja ya kuondoa upweke na uchoshi huo kabisa ni kwa kutafuta njia bunifu za kuwasiliana na marafiki na familia.

Haya hapa ni maoni matatu ya kudumisha umbali wa kimwili huku ukiwa bado umeunganika kijamii… Ujuzi wa mtandao, wezesha!

Simu za kikundi FTW!

Vikundi vya kupiga gumzo ni vizuri, lakini kuna jambo maalum kuhusu kusikia sauti na kuona nyuso. Iwe ni kujuliana hali kwa kila siku au mazungumzo ya upendo ya kila wiki, unaweza kuitumia programu yako uipendayo ya kupiga ngumzo (kama vile Facebook Messenger au WhatsApp) kupanga simu za kikundi za sauti au video na rafiki zako. Simu hizi zinaweza kutokuwa rasmi kama vile muda wa mapumziko wa chakula cha mchana, au unaweza kujaribu jambo lililo na ajenda. Wazo moja? Kuwa na sherehe za kawaida bila mpango maalum — muulize kila mtu atafute ukweli unaoburudisha wa kushiriki na kikundi, na jinsi ukweli huu ulivyo wa ajabu zaidi na wa kipumbavu zaidi, ndivyo ilivyo vyema zaidi! Psst: Je, unajua kuwa iwapo ungeingia garini na uendeshe moja kwa moja juu ukielekeaangani, ingekuchukua saa moja kufika kwenye anga? Ni kweli!)

(Kutengeneza tena) na kushiriki maelezo rahisi ya upishi

Endeleza somo la kupika mkiwa na rafiki zako! Tafuta maelezo rahisi ya upishi kwenye mtandao na kisha uyatengeneze wewe mwenyewe, huku ukiunda video rahisi ya mafundisho kwenye simu yako. Mara utakapokamilisha, shiriki maelezo haya rahisi ya upishi na video na marafiki na uwape changamoto ya kutengeneza aina bora ya chakula chako. Usisahau kuwaambia washiriki picha za chakula chao kwenye kikundi chako cha kupiga ngumzo ili uweze kutoa zawadi za mtandaoni kama 'Juhudi Bora', 'Mpishi Mkuu', na 'Upigaji picha wa chakula wa kuvutia'.

Jiunge na changamoto... au uunde yako!

Mitandao ya kijamii imejaa changamoto: muda wa hadithi, mitindo ya kudensi, mizaha ya kijinga, mbinu za kimaajabu, na mengine. Tafuta changamoto ambayo ungependa kuijaribu na pia uwakaribishe rafiki zako wajaribu. Au, iwapo wewe ni aina ya watu walio wabunifu, unaweza kuwaza na kubuni changamoto yako. (Kumbuka tu kuwa changamoto ambazo zinaweza kumdhuru mtu — kimwili au kihisia! — sio za kuburudisha na sio nzuri.) Shiriki changamoto yako na marafiki na kwenye mitandao ya kijamii na uone jinsi litakavyoenea mbali! Msichana, wewe ni mwanzishaji wa mtindo!

Share your feedback