Sababu 3 kwa nini hauhitaji mvulana

Tayari una yote unayohitaji!

Niko karibu kuanza mwaka wangu wa mwisho katiku shule ya sekondari. Ninataka kuwa Uhandisi wa umeme – kwa hivyo ninahitaji kuhakikisha alama zangu ziko juu. Nina azimio la kutimiza malengo yangu.

Lakini hivi majuzi wazazi wangu waliniambia wanataka niwache shule na niolewe na rafiki wa familia. Wanafikiria ni jambo bora kwa maisha yangu ya baadaye.

Ninapenda masomo yangu na siko tayari kuangazia kuanza familia. Ninajua wananitakia mema lakini nilijua ningewaonyesha kwamba ninaweza kujenga maisha yangu ya baadaye bila mvulana.

Usiku mmoja niliwaketisha chini na nikapitia sababu 3 kwanini sihitaji mvulana maishani mwangu kwa sasa.

Kuangazia masomo yangu ndio ufunguo wa maisha yangu ya baadaye. Niliwaambia wazazi wangu kwamba masomo yangu yanaweka msingi imara kwa maisha yangu ya baadaye. Niliwaonyesha jinsi alama zangu zilivyokuwa bora na nikawaonyesha majibu kutoka kwa walimu wangu kuhusu walivyoniona mwerevu. Babangu alijivunia sana na kupiga tabasamu kubwa sana.

Pesa zangu, maamuzi yangu. Kwenye kazi yangu ya wikendi, ninapata pesa za kutosha kusimamia karo yangu, nikipata ujuzi muhimu vilevile. Kusoma kwa bidii wiki mzima na kufanya kazi wikendi hakubakishi muda wa mvulana. Ninaweza kusoma na nipate pesa zangu mwenyewe, kitu ambacho kinanipatia uhuru wa maisha – badala ya kumtegemea mvulana.

Mifano dhabiti ya mwanamke ni muhimu. Kupitia shule, nilijiandikisha kwa mpango wa ushauri mtaani. Wanawake waliohitimu wanapeana usaidizi kukusaidia kutimiza malengo yako. Mshauri wangu Farah hunisaidia kupanga maisha yangu ya baadaye. Ako katika chuo kikuu akisomea uhandisi na pia anafanya kazi katika kampuni ya umeme. Huwa ninamtembelea pale na ananifunza mengi sana. Kwa usaidizi wake, ninajua nitapata alama za kutosha ili nifanye kozi ninayotaka katika chuo kikuu.

Ninashukuru sana wazazi wangu waliweza kusikiza mahitaji yangu. Sasa nina usaidizi wao niweze kumaliza mwaka wa mwisho na pia wanihimize katika juhudi zangu za kwenda chuo kikuu.

Share your feedback