Uwongo 5 ambazo zitakurudisha nyuma

Ni wakati wa kujichunguza

Siku nyingine unaweza kujihisi vizuri sana, na siku nyingine hutaki kutoka nyumbani au kuonyesha uso wako kwa mtu yeyote. Ni vigumu kujaribu kila wakati kuwa sawa na kile ambacho kila mtu anasema ni kizuri na kinafaa.

Jambo muhimu kuhusu kujiamini na kuwa na furaha kivyako ni kuepuka kuingia katika mtego wa kuamini visasili hivi vitano!

Uwongo wa 1: Kila mtu ako sawa.

Ukweli: Unachoona katika sherehe, shule au kazini, na hasa katika mitandao ya kijamii, huwa si kweli kabisa. Inapofikia wakati wa kujihisi vizuri, jambo muhimu zaidi ni kwamba sisi wote hupata chunusi, sisi wote tuna kasoro, na wakati mwingine sisi wote hujishuku. Cha maana, ni kwamba unajipenda mwenyewe, matatizo yako na kila kitu! Jaribu kuimarisha imani hiyo kwa kurudia kitu kimoja unachopenda kujihusu kila asubuhi.

Uwongo wa 2: Mavazi na vipodozi vitanifanya nijihisi mrembo zaidi.

Ukweli: inafurahisha sana kujaribu vipodozi tofauti. Lakini hisia hizi ni za muda tu. Wewe pia ni mrembo wakati hujajipodoa na wakati umevaa tisheti na mifuto yako ya zamani uipendayo. Kumbuka, kuwa mrembo ndani ndio muhimu. Kubalianeni na marafiki zako mjaribu kukaa siku moja kwa wiki bila kujipodoa!

Uwongo wa 3: Hakuna mtu mwingine uhuzunika kama mimi.

Ukweli: Ingekuwa watu hawahuzuniki, wangekuwa roboti! Ni kawaida kabisa kuwa na hisia tofauti. Ikiwa wewe ni mwaminifu na marafiki zako kuhusu unavyohisi wakati mwingine, wanaweza pia kujifungua kwako pia. Hii itawasaidia kama kikundi kuhimizana na kusaidiana na kukuza imani.

Uwongo wa 4: Kuwa katika uhusiano kutanifanya niwe na furaha.

Ukweli: Wakati una mtu anayekiri mapenzi yake ya dhati kwako kila wakati, kwa hakika hukufanya ujiamini! Lakini kuwa mwanamke anayejiamini na mwenye furaha huanza na wewe.

Uwongo wa 5: Hakuna mtu anayenichukuliwa kwa uzito.

Ukweli: Wakati mwingine uhisi ni kwamba hakuna mtu anayekusikiliza, au kukuelewa, na wanakuchekelea tu, hata wakati unasema ukweli. Ikiwa unahisi haueleweki, jaribu kuchukua hatua mbili nyuma na uangalie hali yako kutoka kwa mtazamo tofauti. Pengine kuzungumza na watu hao kwamba unahisi hawakuelewi kunaweza kusaidia ueleweke zaidi na kukupa ujasiri wa kukufanya uongee wakati una jambo muhimu la kusema.

kwa hivyo wakati mwingine unahisi umenaswa na visasili hivi, jiangalie kwenye kioo na ujiambie: "Mimi ni mrembo, nina nguvu, ninaweza!

Share your feedback