Inaanza na wewe!
Ndoto yangu ni kuwa mwanasiasa, ninataka kufanya mabadiliko katika jamii yangu. Kila wakati mimi huwaona kwenye TV wakizungumza na umati wa watu lakini sijawahi kuwa bora katika kutoa hotuba. Lilikuwa jambo ambalo nilitaka sana kuwa bora..
Imenichukua muda, mazoezi mengi na vikwazo kadhaa – lakini ninajiamini zaidi kuliko hapo awali kuzungumza mbele ya wanafunzi wenzangu.
Nimejifunza vidokezo kadhaa rahisi vinavyonisaidia – kunisaidia kubadilisha woga kuwa furaha na kukaribia mafanikio katika sekunde chache!
Hivi hapa vidokezo vyangu 3 ambavyo unaweza kujaribu katika sekunde 60!
1. Onyesha uwezo wako – hata unapokuwa hujisikii!
Mbinu rahisi ya kuweza kujiamini kwa ndani ni kuhisi mwenye nguvu kwa nje. Nilikuwa najikokota na kufunika mdomo wangu nilipokuwa nikizungumza.
Sasa, kabla sijaenda mbele ya umati, ninachukua muda kujiandaa.
Ninavuta pumzi kwa nguvu, hadi ninapopata nguvu mwili mzima – hadi kwenye ncha ya vidole na kichwani! Jaribu mbinu hii unapokuwa na woga wa kujaribu jambo. Utahisi vyema – pamoja na kuonyesha ujasiri wako utakufanya uweze kufanya vyema pia.
2. Pata wito wako
Wito ni sentensi moja au mbili ambazo hukusaidia kupata nguvu.
Kabla ya hotuba kubwa, mimi husikia woga, lakini natumia wito wangu kujituliza. Wangu ni – ‘Ninajitoa kutoka kwenye hali niliyoizoea ili nitimize ndoto zangu’.
3. Tafuta mtu wako mwenye nguvu
Nilikuwa na wakati mwingi nilipojishuku. Nilidhani sitawahi kuwa bora.
Nilijifunza kwamba wakati mwingine, nilihitaji kuomba msaada.
Rafiki yangu wa dhati Rosamie daima alinikubalia nifanye mazoezi ya hotuba yangu mbele yake – na ananipa maoni ya kweli na ya kusaidia.
Iwe ni mama yako, rafiki yako wa dhati au mwalimu – kutakuwa na watu maishani mwako wanaokuamini. Wafikie watu hawa ili wakukumbushe ujuzi wako.
Kuomba msaada, kujiambia maneno ya kujitia nguvu au kuchukua muda kujitia nguvu hakutachukua dakika moja. Utakuwa umekaribia mafanikio na hatua moja katika muda mfupi!
Share your feedback