Je, Anita anapaswa kusema ukweli kuhusu rafiki yake?
Anita na Sarah walikuwa na umri wa miaka 14 - wamekuwa marafiki tangu utotoni. Siku moja walienda pamoja kununua bidhaa sokoni na kuona viatu vyekundu maridadi vilivyong'aa. Sarah alipenda viatu hivyo lakini hakuwa na pesa za kutosha za kuvinunua. Wakati ambapo hapakua na mtu anayeangalia alivificha haraka mfukoni mwake. Anita alishtuka na alihisi vibaya sana. Alishangaa kwa nini Sarah alifanya jambo kama hilo. kufanya hivyo.
Kuiba huwa si wazo nzuri na kama Sarah alitaka viatu hivyo alifaa kuhifadhi pesa ili aweze kuvinunua. Sarah alimsihi asimwambie mtu yeyote na wote wakatoka sokoni na kwenda nyumbani.
Anita alipofika nyumbani alionekana amekasirika na mwenye wasiwasi. Alikuwa na wasiwasi sana kuwa huenda kuna mtu alimwona na kwamba anaweza kuwa matatani kwa sababu ya Sarah. Mama yake Anita aligundua kuna jambo baya na akamuuliza ni nini kilichofanyika lakini Anita hakuwa na lakusema kusema. Upande mmoja alikuwa na hofu na alihisi anapaswa kuwa kimya. Upande mwingine alitaka kuwa mjasiri na kusema ukweli.
Lakini wana Springster, mnafikiria Anita alifanya nini? Alisema ukweli! Kusema uongo kunaweza kuonekana ni kama njia rahisi, lakini hurejea tena na kukusumbua. Huenda kusema ukweli ikawa vigumu lakini angalau ndio jambo sahihi la kufanya.
Iwapo utawahi jipata katika hali kama hii, hapa kuna baadhi ya vidokezo vya kuongea na mtu kuihusu:
1. Ongea na mtu mzima unayemwamini
Anita alikuwa sahihi kuongea na mama yake badala ya kujiwekea hisia zake mbaya kivyake. Kabla ya kufunguka, kumbuka kufikiria vyema unachotaka kutamka na uwe mtulivu unapokuwa ukijieleza.
2. Kuwa mwaminifu kuhusu hali hiyo.
Kusema ukweli huweza kukuletea imani , na imani kati yako na wazazi wako ni muhimu. Kupata usaidizi wa baadaye ni rahisi pia wakati watu wanajua wewe ni mtu mwaminifu.
3. Wajibika kwa hatua zako.
Jaribu usishawishiwe na watu wa rika lako, lakini ukifanya kitu kibaya, wajibika kwa hatua zako na uombe msamaha.kutamka neno “pole” husaidia sana.
4. KUWA MKAKAMAVU na MJASIRI.
Ukiona kitu kibaya, usiogope kuripoti. Daima jambo la haki. Mwishowe utanufaika. .
Mwishowe mama ya Anita alilazimika kuongea na mama yake Sarah na Sarah alirejesha viatu hivyo na kujifunza somo . Mwanzoni Sarah alikuwa amemkasirikia Anita lakini mwishowe akagundua Anita alikuwa rafiki mzuri.
Share your feedback