Ujuzi wa ajabu ulionao tayari

Sauti yako ni muhimu

Hebu fikiria mtu mwingine akikuamulia ni vazi gani nzuri la kuvaa, aina ya muziki wa kusikiliza au hata unachofaa kusomea.

Kwa bahati mbaya, huu ni ukweli kwa wasichana wengi. Wakati mwingine tunahisi kama maoni yetu sio muhimu na hatutaki kuzungumza. Mara nyingi tunahisi hivi kwa sababu tunaambiwa na familia na marafiki tunyamaze, tuzungumze kwa upole na utulivu.

Hata hivyo, niko hapa kukuambia unaweza kuwa mtulivu na mwenye urafiki na bado uweze kutoa maoni yako ya dhati. Bila shaka, wasichana tayari wako na ujuzi unaohitajika kuzungumza hadharani, wanahitaji motisha kiasi tu.

Mambo muhimu kwanza, wasichana wana maoni!

Ingawa wasichana wengi ni wenye kuzungumza sana miongoni mwa wenyewe, wao hupata ugumu kuzungumza hadharani. Mara nyingi, tuna woga wa kuzungumza maoni yetu hadharani kwa sababu tunaogopa kuchekwa. Hata hivyo, ni muhimu kupatia watu mitazamo tofauti na nani anajua: unaweza kubadilisha fikra za mtu. Jambo la muhimu ni kujua utakachokisema na mbona wataka kukisema.

Jifanye hadi ufanikiwe

Kuzungumza hadharani kunahitaji ujasiri, lakini hii sio rahisi kila wakati. Hata hivyo, unaweza kujifanya una ujasiri, hata kama huna. Hakuna anayeweza kusoma fikra zako kwa hivyo hawatajua na watakachokiona ni mtu anayetaka kuzungumza. Pia, kadiri ‘unavyojifanya’ inakuwa rahisi kuzungumza. Utajipata ukiwa jasiri zaidi!

Fanya mazoezi

Kadiri unavyofanya jambo, ndivyo utakavyokuwa bora. Kwa hivo usife moyo unapopata wasiwasi au unaposahau ulichotaka kusema mara ya kwanza kuzungumza. Itakuwa rahisi kadri muda unavyosonga.

Kumbuka, kuna mambo mengi ambayo sisi wasichana hufanya ambayo huashiria nguvu zetu. Kwa hivyo, hata kama kuzungumza hadharani kunakaa kugumu, una uwezo wa kufanya hivyo.

Share your feedback