Damu ni nzito kuliko maji

Familia ndiyo muhimu zaidi.

Kukutana na kujua watu wapya nje ya familia yetu ni jambo la kusisimua na bora zaidi na mduara huu wa marafiki unaendelea kupanuka tunapozeeka na kukutana na watu zaidi wanaovutia na waungwana.

Ukiwa kijana, utafahmu kuwa watu wengine katika mduara wako ni waungwana zaidi wa kutangamana nao kuliko wazazi wako wanaoudhi na kukasirisha wakati mwingine. Tukiwa wachanga, tunaonekana kuwa na shughuli nyingi na kuishi maisha yetu binafsi hivi kwamba tunasahau kuwa wazazi wetu wanazeeka. Ingawa linaweza kuwa jambo la kushawishi kukumbana na hali mpya na kufurahia na vijana, mwishowe, wazazi na familia zetu ni watu wanaotukubali na kutupenda bila masharti. Watu watakuja na kuenda, lakini familia ni ya milele.

Hatusemi lazima ukae na wazazi wako kila wakati (hilo litakuwa la ajabu!), lakini kuna njia rahisi za kuhakikisha kuwa wazazi wako ni sehemu ya maisha yako:

Wahusishe
Ni rahisi kama kuwaambia kuhusu matatizo yako au hadithi kuhusu kile ambacho marafiki zako wanafanya. Waombe ushauri kuhusu mada tofauti, wana tajiriba nyingi sana ya maisha na wanaweza kukupa mtazamo mpya. Wazazi wako waliwahi kuwa wachanga pia! Wataelewa unachopitia.

Kuwa karibu
Baba anatatizika kukarabati gari? Msaidie na upate muda bora kwa muziki. Unaishi mbali na wazazi wako? Wapigie simu, si lazima liwe tukio kubwa, lakini kuangalia tu kunaleta tofauti kubwa. Unatumia wiki nzima kushughulikia mambo yako, kama vile shule na marafiki, unaweza kuchukua dakika 15 wikendi kuwasiliana na mama yako, alikupa muujiza wa maisha!

Njia nyingine ya raha kuwa nyumbani ni kwa kuchanganya dunia zako mbili. Waalike marafiki zako kula pamoja au kutangamana tu na familia yako. Sifa zaidi: hii itaonyesha familia yako kuwa marafiki zako ni watu wazuri unaowajali pia. Ni marafiki zako, sio tu watu wowote.

Wajibika
An ana miaka 19 na anajitenga na mama yake. Ani anataka kuwa huru na kukomaa na hatimaye kuwa mtu mzima ambaye amekuwa akitamani kuwa. Kuna kitu kimoja pekee kinachomzuia: mama yake. Humwona Ani kama mtoto. Lakini badala ya kulalamika kulihusu, Ani aliamua kuchukua hatua na kumwonyesha mama yake kuwa angeweza kujitegemea zaidi maishani mwake. Kwanza, alihakikisha kuwa alama zake na kazi ya shuleni vilikuwa sawa, kisha akasaidia nyumbani na hata kuanza kazi ya muda wa ziada. Haijawa rahisi, lakini mama wa Ani ameanza kuona kuwa Ani anakua mwanamke mchanga mwerevu na anayewajibika. Hata uhusiano wao ni bora zaidi kuliko awali!

Share your feedback