Fanya kinachokupendeza... pata kuungwa mkono na wazazi!

Tumia maneno 3 haya ya ajabu

Pria alikuwa na umri wa miaka 14 alipoanza kupenda muziki. Siku moja alipokuwa akielekea nyumbani kutoka shuleni alisikia muziki wa kuvutia zaidi kutoka kwenye jengo la mbali. Alifuata sauti iliyomwelekeza kwenye barabara nyembamba kwenda katika jengo. Hapo alipata kundi la vijana kama yeye waliokuwa wakiimba na kucheza vyombo mbalimbali. Alipendezwa sana.

Pria alikuwa akichungulia akiwa katika kona ili asionekane. Alitambua kuwa kiongozi wao alikuwa mwalimu wake wa sayansi kutoka shule. Haya yanashangaza aliwaza. Alikuwa anafanya nini kufunza muziki? Ghafla simu yake ikaanza kuita. Mame yake alikuwa anapiga simu. Kelele ya sauti ilimfanya ajulikane, hivyo aliruka juu na kuondoka mbio.

Siku iliyofuata katika darasa la sayansi mwalimu wake, Bwana Rajen, akamwuliza, "Je, huyo alikuwa wewe, Pria, nilikuona ukichungulia darasa langu la muziki jana?” Pria alitingisha kichwa chake

"Ungependa kujifunza kucheza chombo cha muziki?" Aliuliza Bw. Rajen.

Pria alitambua upendo wake wa muziki ulikuwa mwingi sana. Alikuwa na hamu ya kuchunguza shauku hiyo kwa hivyo akasema ndiyo. Hata hivyo ingechukuwa kazi kubwa ili kuwashawishi wazazi wake.

"Sidhani wazazi wangu wataniruhusu," Pria akasema kwa sauti ya chini.

Kisha Bw. Rajen alimpa Pria ushauri wa jinsi ya kuungwa mkono na wazazi au walezi.

1. Kujitolea

Unapokuwa mdogo ni rahisi kuchanganyikiwa. Kila kitu huonekana cha kufurahisha na cha kusisimua, lakini huwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja. Ikiwa wazazi wako watawekeza fedha katika masomo ya muziki wanahitaji hakikisho kuwa utaendelea na hutakufa moyo ikiwa utaboeka. Wakumbushe mara ambazo umejitolea.

2. Shauku, shauku na shauku zaidi

Onyesha wazazi wako jinsi ulivyo na shauku ya kujifunza chombo cha muziki. Zungumza nao kuhusu jinsi unavyopenda muziki. Zungumza nao kuhusu jinsi muziki unavyokusisimua na kuwashawishi kuwa una uwezo wa kuwa mwanamuziki bora.

3. Shiriki maono yako

Unatarajia kunufaika vipi kutokana na kujifunza chombo kipya? Shiriki nao! Waonyeshe ujuzi wote mpya utakaojifunza na fursa zote mpya ambazo zitatokana na muziki. Hasa fursa za kifedha. Pia zungumza jinsi inavyoweza kuathiri maisha yako ya baadaye kwa njia nzuri.

Huenda hauna haja ya kujifunza kucheza chombo, lakini vidokezo hivi vinaweza kutumika katika mradi wowote unaotaka kutekeleza.

Share your feedback