Kushindwa kunaweza kuwa jambo nzuri kwako

Jifunze jinsi ya kuinuka wakati maisha yanapokuangusha chini!

“Na tuunde mustakabali wetu sasa na tufanye ndoto zetu za kesho kuwa kweli”

Maneno haya yalisemwa na Malala Yousfzai, mwenye umri wa miaka 18 mshindi wa Tuzo la Amani la Nobel na mtetezi wa haki za elimu kwa wasichana. Malala alishinda vikwazo vyote na kuwa mmoja wa sauti zinazoongoza za kizazi chake.

Hadithi yake imewahimiza wasichana wengi wadogo kutetea wanachokiamini na kufikia ndoto zao haijalishi ni mara ngapi wanashindwa.

Wakati fulani katika maisha yetu tutashindwa kufanya kitu. Lakini cha muhimu ni jinsi tunavyoangalia kushindwa; je, tutaingalia kama ishara kwamba tumeshindwa na kulaaniwa au tutachagua kujifunza kutokana na tukio hilo?

Hapa Springster tunachagua chaguo la pili. Njia nzuri ya kujiinua baadhi ya kushindwa au kufa moyo ni kutafuta somo ndani ya tukio hilo. Jifikirie, ni nini ninachoweza kufanya wakati mwingine ili kuhakikisha nimepata matokeo bora? Nilipata aje matokeo haya kwanza?

Angalia vidokezo hivi ili kukusaidia kuinuka baada ya kuanguka:

  1. Kubali: Kwa hivyo mambo hayakutokea kama ulivyopanga na hiyo ni sawa, hutufanyikia kwa sisi wote. Ishara ya shujaa wa kweli ni mtu ambaye anayeweza kukubali makosa yake na kisha kujaribu kujifunza kutokana na makosa hayo.

  2. Ng'amua zaidi: Chukua muda kuelewa ni nini ambacho hakikufanyika kulingana na mpango. Pengine hukuchukua muda wa kutosha kusoma au hukupiga hesabu zako vizuri. Ukielewa jinsi mambo yalivyokwenda mrama itakuwa rahisi kufahamu vyema.

  3. Tekeleza: Kwa kuwa sasa unaelewa ni nini kilichofanyika ni wakati wa kuweka pamoja mpango wa kuhakikisha mambo yanafanyika vizuri wakati mwingine. Iwe ni kuchukua muda zaidi kusoma au kupunguza gharama zako za biashara - chochote kile, anza kuzitekeleza mara moja ili uweze kukaribia ndoto zako.

  4. Endelea kupata msukumo: Endelea hadi uifahamu, kwa sababu mwishowe kila kitu kitakuwa sawa.

  5. Usiwe na vizingizio: Kuwa mkweli kwako kuhusu matatizo yoyote na uyatumie kama mafunzo na jiwe la kukanyagia kwenye njia yako ya ufanisi.

Je, uko tayari kuanza kutimiza ndoto zako kama malkia kwa kujifunza kutoka kwa kushindwa kwako? Endelea hivyo!

Share your feedback