Usihofu ni kawaida!
Umewahi kujikuta unalia pasipo sababu yoyote? Au kifua kinabana na unasikia mgandamizo juu yako
Unaweza pia kujisikia kuwa mpweke muda mwingi na kufikiri mawazo mabaya juu yako. Usijali! Ni sawa kuhisi kama hivi wakati mwingine. Hauko peke yako na wewe ni wa muhimu
Tunapokua tunakumbana na hisia za kila aina. Wakati mwingine tuko juu, kisha tunakuwa chini, halafu tunarudi tena juu. Rafiki yangu Lewa alikuja kwangu wiki iliyopita akihisi yuko chini. Niliweza kumsaidia kwa sababu nilikuwa najiskia vivyo hivyo mwezi uliopita. Uzuri wa hisia mbaya ni kwamba kila kukicha hupita. Mwezi uliopita nilijihisi mnyonge lakini sasa nimeweza kutumia kile nilichojifunza kumsaidia rafiki yangu.
Huu ni ushauri niliompa unaoweza kukusaidia na wewe pia.
1. Daima kumbuka kwamba hauko peke yako. Sisi sote tuna uzoefu sawa wa furaha na huzuni. Ni sehemu ya asili ya maisha. Hatuwezi kuwa na furaha wakati wote na hatuwezi kukaa na huzuni milele. Ikiwa unahisi kuwa chini kumbuka una Springsters na Dada Wakubwa wenzako ambao unaweza kuja hapa na kuzungumza nao. Unapaswa pia kuwa muwazi kwa wenzio kuhusu jinsi unavyohisi, huwezi kujua nani anaweza kukusaidia.
2. Kuwa na mpango wa furaha. Tunapopitia kipindi cha baleghe hisia zetu ziko kila mahali. Kwa hiyo katika maandalizi kwa ajili ya siku mbaya unaweza kutengeneza mpango wa furaha wa mambo yote unayoweza kufanya ili kujifurahisha na kujisikia vizuri zaidi. Kwangu, shughuli zangu zilihusisha kuwa na marafiki. Kama kuogelea na Amira au kuoka keki na Cecile. Kufanya mambo unayopenda na watu unaowapenda hufanya uhisi kuwa bora zaidi kwa haraka.
3. Jifunze kushukuru. Siku mbaya haimaanishi maisha mabaya hivyo daima jaribu kutizama picha kubwa. Kuandika chini vitu 5 unavyoshukuru kwavyo kila siku kunaweza kukuweka katika hisia ya ajabu.
Kwa ujumla kuzungumza na marafiki husaidia sana kwa sababu unatambua haraka kwamba hauko peke yako katika kile unachopitia, na kama wasichana wengine wanaweza kustahimili basi hata wewe unaweza.
Share your feedback