Kazi za kinyumbani si za wasichana pekee

Nilitoa changamoto “jinsi mambo hufanywa wakati wote”

Nilipokuwa mdogo, nilifurahi sana wakati familia yote ilipokutana nyumbani kwetu. Mimi na binamu zangu tulicheza michezo ya kusisimua nje. Mimi na ndugu yangu Tony tulitengeneza timu nzuri wakati wote. Nilipoendelea kuwa mkubwa, nilianza kutambua kwamba nilitumia muda mdogo nje na muda zaidi jikoni pamoja na mama. Tony, kwa upande mwingine, bado aliruhusiwa kucheza. Hakuna aliyemhitaji jikoni kusaidia. Hilo lilinishangaza - hivyo nikaulizia kuhusu jambo hilo. Nilimwuliza mamangu sababu ya kutonikubalia kwenda nje na kubaki ndani nikiosha vyombo. Yale aliyosema ni, "Hivyo ndivyo mambo yalivyo.”

Hmmm niliwaza - 'kweli, inapaswa kuwa hivyo?' Hakuna aliyetaka kujua nilivyohisi au nilichotaka. Nilitarajiwa tu kutii sheria. Sikilizeni, Wana Springster: Maamuzi yanapofanywa na huoni kama yanazingatia maslahi yako, una haki ya kuuliza maswali. (Lakini tu ikiwa unahisi ni salama kufanya hivyo, bila shaka!)

Katika hali hii sikuona utofauti wangu na Tony, kwa hivyo nikauliza maswali. Mamangu hakuwa na mtazamo mpya wa kufanya mambo, hivyo nikaenda kuzungumza na Tony jioni wakati kila mtu ameondoka. Nilimweleza jinsi nilivyokosa kuwa mwanatimu pamoja naye na ikiwa angenisaidia kwa dakika chache labda tungeweza kufanya mambo kwa haraka zaidi. Pia nilijitolea kumsaidia kwa kazi yoyote ambayo angetakiwa kufanya.

Wakati watu walipokuja kututembelea tena, wazazi wangu walishangaa walipoona mimi na Tony tukiosha vyombo pamoja. Sasa imekuwa kama tamaduni mpya nyumbani kwetu. Hakuna sheria eti kazi za nyumbani ni za wasichana pekee. Mimi na ndugu yangu tunafanya kazi pamoja na kutengeneza timu nzuri. Najivunia sana hatua yangu ya kupinga na kuongea kuhusu ubaguzi huo.

Sisi wasichana tunastahili uhuru sawa na mtu mwingine yeyote. Hivyo ikiwa yeyote atajaribu kuzuia matendo yako: Simamisha. Waza. Jiamini. Na kupinga mawazo yao. Ikiwa ninaweza kufanya hivyo, basi unaweza pia. Ikiwa unampinga mtu mkubwa kukiko wewe, kumbuka kubaki kuwa mtulivu na kuwa na heshima.

Share your feedback