Si wewe! Ni mimi!

Jifunze jinsi ya kukabiliana na watu ikiwa wewe ni mndani.

Mikono juu ikiwa uko kwenye Kilabu cha Wandani!

Wewe ni mndani ikiwa...unahisi una nguvu unapotumia muda wako peke yako, kupata nishati. Unataka kutenga muda wa kuwa peke yako, kufanya mambo yako unayopenda: kusoma, kufuatilia vipindi, kuchora au kupanga chumba chako.

Wandani wote hukaa tu kwenye nyumba siku nzima? Haiwezekani! Unaenda nje na kufurahia. Unafurahia kwa njia tofauti.

Kuwa mndani hakukufanyi kutotangamana. Ni kwamba...wewe ni mtu unayefurahia kuwa peke yako. Na hakuna tatizo na hilo!

Kuwa mndani wakati mwingine huwa kugumu, kwa sababu dunia nzima inapenda wasondani. Wasondani hupata nguvu zao kupitia kutangamana na kutumia muda wao na watu wengine. Wandani na wasondani ni kinyume cha mwenzake

Utakabilianaje na watu ikiwa wewe ni mndani? Jambo la kufanya marafiki zako wanapokufanya uhisi kuwa na hatia kwa sababu umepata kitabu kizuri zaidi na kutumia usiku mzima kupiga gumzo kinaonekana kama kitu kibaya zaidi? Kitu cha kufanya unapowataka wajue kuwa unajali na hutaacha kujali?

Vyema, huna budi kuionyesha. Ikiwa marafiki zako wanakujua vyema zaidi, wataelewa. Na wasipokuelewa? Waelezee. Onyesha kuwa unajali kwa njia nyingine. Andika barua au tuma vifurushi kadhaa vya kujali. Linafanya kazi. Ungana na watu kwa njia ambayo ni ya kweli ya kuonyesha ulivyo.

Badala ya kupoteza roho yako kwenye jumba la biashara, waalike marafiki zako kwenye bustani au kijia cha asili. Wafanye watu waelewe mambo unayopenda — na uone uhusiano wako na watu maishani mwako ukiwa wa ndani na wenye maana.

Kuwa mndani kunamaanisha kuwa umetumia muda mwingi sana kutafakari wewe ni nani, kwa hivyo simamia hilo. Jua wewe ni nani, kuwa wewe, na usambaze furaha kwa watu unaowajali — fanya tu kwa njia ya kawaida!

Share your feedback