Kuzungumza kunaweza kubadili maisha yako

Usijisikie mnyonge mbele ya matatizo.

Wakati mwingine, tunapokabiliwa na tatizo, inahisi kana kwamba kuna ukuta mbele yetu ambao unakua kila siku. Kupita kwenye uwazi wa tofali moja tu inaonekana haiwezekani - na wenye kutokuwa na maana wakati ukuta huo unaonekana kuwa mkubwa sana.

Lakini ikiwa unaweza kuchukua hatua hiyo ya kwanza ya ujasiri na kukabili tatizo lako, unaweza kushangaa jinsi mambo yanavyoweza kuanza kuwa mazuri kwa haraka.

Tatizo la pamoja
Katika shule anayosoma Kara, hapakuwa na vyoo vizuri. Hakuna vyumba binafsi, hakuna masinki ya kuosha mikono yao. Wakati yeye au wasichana wengine katika darasa lake walipokuwa wanapata hedhi zao, walilazimika kutembea kwa maili kufikia choo kizuri.

Hasira kwa vitendo
Alipokuwa akienda kwenye vyoo siku moja, Kara alihisi hasira. Alikuwa anakosa kipindi chake alichokipenda. Na mmoja wa marafiki zake hakuja shuleni wiki hiyo nzima kwa sababu alikuwa na aibu sana.

Alikasirika vya kutosha. Haikuwa haki - wavulana hawakuwa na shida juu ya hili, na wasichana walishindwa kwenye masomo hata kama walikuwa werevu na wenye bidii. Hasira aliyohisi ilimuondolea aibu yake na haya yake. Kabla ya kupoteza ujasiri wake, aliamua kwenda kwa mwalimu wake.

Nguvu kwa idadi
Mwalimu wa Kara alikubali kuwa kitu kinapaswa kufanyika, lakini alipendekeza Kara akusanye kundi la wasichana kuthibitisha kuna shida katika darasa lote. Kisha, wote pamoja, wangeweza kwenda kwa mwalimu mkuu na kuelezea ni mara ngapi walikuwa wanakosa masomo.

Kujenga kwa imani
Wasichana waliweza kumshawishi mwalimu mkuu. Pamoja walijitahidi kuandaa tukio la kukusanya fedha, kwenda kwa makundi ya wanawake wa mitaa na vituo vya jamii kukusanya msaada waliohitaji.

Wasichana walijenga ujuzi wao na ujasiri wao. Na hatimaye choo kilijengwa pia. Kila wakati wasichana walipokitumia waliona fahari, wakijua kuwa kilikuwapo kwa sababu walikuwa na ujasiri wa kuzungumza.

Rejelea masomo
Bila shaka jibu la tatizo unalokabiliana nalo siku zote haliwezi kuwa wazi kama kukusanya fedha kwa ajili ya jengo. Lakini kuanza kwa kushirikishana, na kuungana na wengine ambao wanaweza kuwa wanakabiliwa na tatizo hilo, mara nyingi ni mwanzo mzuri wa kuvunja kuta hizo tunazoweza kukabiliana nazo. Kila la Kheri!

Share your feedback