Kuendelea kuwa na nguvu baada ya wazazi wangu kuwachana

Niligundua ilikuwa vigumu kwetu sisi sote.

Miaka michache iliyopita, mambo yalikuwa magumu sana nyumbani. Wazazi wangu walipigana sana na hatimaye waliachana na baba yangu akaondoka. Ilikuwa ngumu kwetu sisi sote, hasa mama yangu. Alihitajika kunitunza mimi na ndugu zangu wawili wadogo pekee yake, akiwa anaendelea kufanya kazi.

Ilibidi sisi sote tuzoee maisha bila baba yetu. Kama mkubwa wao, nilisikia kuwajibika kumsaidia mama yangu nilipoweza, lakini nilichoweza fanya pekee ni kugombana naye na kulia kwa ajili ya hali yetu. Hii haikufanya mambo kuwa bora. Hivi karibuni nilianza kutambua kwamba kununa hakungetatua chochote na kwamba sio mimi tu nilisikitika na kujaribu kukabiliana.

Hivyo nilibadilisha mtazamo wangu. Mchana mmoja niliamua kumsaidia ndugu yangu mdogo na kazi yake ya ziada ya nyumbani, nikifanya yangu. Alihisi kuwa wa muhimu kuketi kando yangu na nilijisikia vizuri kujua kwamba mama yangu hangetakiwa kufanya naye alipofika nyumbani kutoka katika siku ndefu kazini kwake. Niliendelea kumsaidia na mama yangu alisema anashukuru sana. Pia nilijitolea kufanya zamu na mama yangu kumsomea mdogo wangu hadithi za wakati wa kulala na nikaanza kusaidia jikoni wakati wa chakula – kuandaa meza, kukata mboga na kuosha sahani. Hata nilimwuliza shangazi yetu anionyeshe baadhi ya mapishi rahisi ambayo ningeweza kutayarisha kwa chajio ili kumpa mama yangu mapumziko ya muda kwa muda. Ilikuwa nzuri sana kumshangaza na chajio mezani alipoingia mlangoni!

Mambo ni bora zaidi nyumbani sasa – na uzuri ni kwamba mama yangu na mimi tuna urafiki wa karibu zaidi kuliko awali. Bado tunamabishano muda kwa muda, lakini tumesaidiana pamoja ili tupate kutoka katika kipindi kigumu sana. Haijalishi kinachotokea sisi tuko pamoja daima.

Nimejifunza kuwa familia ni muhimu, na ikiwa sote tutakuwa chanya na kufanya kazi pamoja, tunaweza kupita kutoka katika kitu chochote.

Share your feedback