Siri ya kuwa na ari kuu

Jiamini wewe mwenyewe

Je, maisha yangekuwa yanasinya kiasi gani endapo watu wote wangefafana kitabia?

Hakuna mwingine kama wewe mrembo - na hiyo ndiyo nguvu yako kuu. Upekee wako ni kitu cha kusherehekea kwa hiyo usifiche asili yako ndipo uweze kuingiliana na jamii. Wakati wote watu watakuwa na maoni fulani juu yako lakini kuwa mkweli wa jinsi ulivyo ndiyo siri ya kuwa na ari kuu.

Kutokana na shinikizo nyingi ambazo sisi wasichana hukumbana nazo siku hizi, ni rahisi kupotea katika hali yetu ya kutokuwa salama na kuishia kutenda yale watu wanataka tutende. Ili uweze kuishi kwa kujiamini lazima uwe na uhafamu mzuri wa wewe ni nani na kile unachopenda kufanya..

Hatua 1- Jitambue wewe u nani

Haya yanahusu uwezo wako na udhaifu wako Je, kiasilia wewe una uwezo wa kufanya mambo gani? Je, unafaulu katika mambo gani? Pengine wewe ni mtalaam wa hesabu au mchoraji mzuri au unaweza vyote viwili! Ni muhimu kujua kile unachoweza kukifanya vizuri na ukifanye kitu hicho kwa sababu kinajenga kujiamini kwako. Pia, unapojua udhaifu wako unaweza kuudhibiti vizuri zaidi na kujifunza kufanya maamuzi mazuri ambayo yanakufanya uhisi ndani yako uko salama.

Swali lingine la kujiuliza mwenyewe ni - nini hukutia nguvu? Mambo mengine yanaweza kukufanya uhisi umechoka sana ilhali mengine yanakupa nguvu na kukufanya uhisi uchangamfu. Je, unajua mambo haya ni yapi? Ikiwa huyajui, anza kufikiria na utafute mambo yale hukusisimua.

Hatua ya 2 - Tambua kile unachop enda na ukifanye

Kufanya kile kinachokupa furaha ni njia nyingine ya kudumu ukiwa mhalisia na mwenyewe. Ikiwa kucheza dansi kunakufurahisha basi cheza dansi utakavyo dada! kiwa marafiki wanakufanya uhisi vibaya juu yako, basi jitenge nao na utafute wengine wanaokupa fursa ya kuwa mwenyewe. Kufanya kitu unachopenda hukufanya uhisi kujiamini na unapokuwa unajiamini uwezo wako hautakuwa na mpaka.

Kufuata ndoto zako kunaweza kukufungua macho ujione ukiwa mwenyewe. Hiyo ni kwa sababu ndoto zetu msingi wake ni yale mambo tunayoyapenda sana mioyoni mwetu. Kila mtu ana ndoto tofauti kwa maisha yao kwa hiyo hakikisha unachukua hatua ili utimize ndoto zako. Ikiwa ndoto yako ni kuanzisha biashara yako basi anza kutenga pesa ili uianzishe; kwa sababu ukifanya hivyo hutawezwa kusitishwa na chochote.

Share your feedback