Kifuatiliaji cha hisia kinaweza kuwa kitoaji kamili cha hisia mbaya ya COVID-19
Taarifa hizi zote kuhusu COVID-19 hunifanya kuwa na wasiwasi! Ingawa ninajaribu kutumia nguvu zangu kwa njia nzuri mchana wote na usiku kuwafanya watu walio karibu nami kufurahi, siwezi kudanganya kuhusiana nayo. Hii sio burudani. Ningependa iishe.
Hivyo la kufanya ni lipi? Kujijali, hivyo tu! Huu ndio muda sahihi wa kujijali zaidi kwa ustawi wako, na hakuna namna nzuri zaidi ya kujijali kama kuwa mwaminifu kwako mwenyewe.
Njia yangu? Uko tayari?! Kitabu cha Kifuatiliaji cha Msingi cha Hisia!
Kifuatiliaji cha Msingi cha Hisia ni kama jarida la unavyohisi wakati wowote. Andika kwenye jarida mara moja kwa siku, mara moja kwa wiki au hata mara tano kwa siku! Chochote ambacho kitakusaidia kuhisi vyema zaidi. Hii hapa ni baadhi ya taarifa ambayo ni ya ya msaada kwa ninayoandika.
Unapotazama kila ulichochora baada ya kingine, labda utaona mengi ambayo wengi wetu huona. Baadhi ya siku kwa kweli huwa mbaya sana, baadhi ya siku ni nzuri, baadhi ya siku huwa blaablaa kabisa. La muhimu zaidi, hata hivyo, utaona kuwa mema husawazisha mabaya, na hata mabaya yalipotokea, uliweza kuendelea.
Kitabu cha Msingi cha Kufuatilia Hisia sio kwa ajili ya kuandika tu kilichotokea. Ni hadithi ya karantini yako na jinsi ulivyoipitia. Ni cha kipekee na ni chako.
Hebu tushiriki vidokezi hivi vya msingi kwa rafiki zako au mtu anayevihitaji zaidi. Tuko pamoja katika hili!
Share your feedback