Kuna watu wazima ambao unaweza kuwaamini
Jina langu ni Satu. Nina umri wa miaka 13. Wazazi wangu wanaishi katika kijiji kidogo. Hawangeweza kunishughulikia mimi na ndugu zangu 4. Kwa hivyo nilikuja kuishi na shangazi na mjomba wangu jijini. nimekuwa hapa tangu Juni mwaka uliopita. Nilikuwa mpweke sana nilipokuja jijini mara ya kwanza.
Shangazi na mjomba wangu wana watoto watatu wakubwa wa kiume. Shangazi yangu husafiri sana kwa ajili ya biashara yake. Kwa hivyo sikuwa karibu sana naye. Nilihisi sikuwa na mtu wa kuongea naye. Nilipoanza hedhi yangu mwezi uliopita, sikujua nimweleze nani.
Kisha nikakutana na Rita! Alijiunga na shule niliyokua muhula uliopita na akawa anakaa kando yangu. Nilijawa na furaha sana. Yeye ni mzuri sana na mwerevu pia. Mimi humwelezea kila kitu. Hata wakati nina matatizo kuhusu wavulana shuleni.
Kwa kuwa sisi ni wa rika moja, Rita alisema hawezi kunisaidia na chochote. Alisema ninahitaji mtu mkubwa wa kuongea naye. Alisema ninapaswa kuongea na shangazi yangu. Kwa kuwa shangazi yangu husafiri sana haimaanishi hatuwezi kuwa karibu. Alisema nimjaribu kabla ya kufa moyo kabisa. Niliogopa kidogo, lakini nikamweleza shangazi yangu kuhusu hedhi yangu wiki iliyopita. Alikuwa mzuri! Alinielezea kuhusu kilichokuwa kikifanyika mwilini mwangu. Hata mambo mengine Rita hakujua!!
Rita alinionyesha kwamba nisiogope kushiriki matatizo yangu. Kwa kawaida watu wazima huwa tayari kusaidia, unachopaswa kufanya ni kuuliza! Hata kama shangazi yangu hayuko, sasa ninaweza kuongea na mshauri katika shule yetu. Nimewapata watu ninaoweza kuwaamini. Hata binamu yangu mkubwa, Mark. Wakati mwingine, huenda kwake kupata ushauri kuhusu wavulana na hufanya mambo kuwa rahisi sana kuelewa.
Sasa najua sipaswi kunyamaza ikiwa kuna shida. Ikiwa una tatizo na unahitaji mtu wa kuongea naye, jaribu vidokezo hivi:
Watu wazima wana hekima na uzoefu mwingi kwa hivyo usione haya. Wana majibu!
Share your feedback