Vitu hivi 5 vinaweza kutatiza ndoto zako
Dada mkubwa mwenye hekima alisema, "Ikiwa unaweza kuiota, unaweza kuipata". Ni rahisi kusema kuliko kufanya, lakini ni kweli. Sisi sote tuna ndoto na matarajio maishani lakini si kila mtu huyatimiza. Baadhi ya watu hukua na huishi i maisha kulingana na ndoto zao wakati wengine wana huzunika kwa sababu hawakuchukua hatua kuhusu ndoto zao.
Uko hai kwa sababu fulani, na kila msichana ana moyo hai wa ubunifu ndani yake. Ubunifu huu, pamoja na usaidizi kutoka kwa watu karibu na wewe, unaweza kufanya ndoto zako kuwa kweli. Kwa hivyo kuwa mwangalifu kwa vitu tunavyosema vinaweza KUIBA NDOTO.
Baadhi ya vitu maishani vinaweza kuiba ndoto zako na kukuzuia usiweze kufanikiwa, kinyume na unavyotarajia. Vitu hivi ni:
1. Hofu – Hofu ni akili yako kufikiria mambo yote ambayo yanaweza kwenda vibaya. Lakini kumbuka Springsters wana nguvu na wana uwezo wa kufikiria mambo yote ambayo yanaweza kwenda SAHIHI. Kwa hivyo badala ya kufikiria je, nikishindwa? Fikiria na je, nikifanikiwa?
2. Kujishuku – Kuwa na imani ndio jambo muhimu la kutimiza ndoto zako. Kujishuku hukufanya uwe wastani na ukwame. Lakini kujiamini hukufanya uwe wa kipekee na hukufanya ufanikiwe.
3. Watu wenye fikra mbaya – Si kila mtu ataamini ndoto yako. Watu wanaweza kusema mambo mabaya lakini usiyazingatie. Bora tu uwe unajiamini, hilo ndilo jambo muhimu, kwa hivyo fuatilia ndogo zako! Usiruhusu wanaokuchukia kukurudisha nyuma.
4. Kukosa motisha – Usiruhusu visingizio kuingia kati! Wakati mwema ni kuchukua hatua SASA. Motisha huja unapoanza, si kabla (ninajua inakanganya lakini niamini). Ikiwa ndogo yako inaonekana kubwa sana, anza na kitu kidogo. Hatua ndogo husababisha mafanikio makubwa!
5. Vikwazo – Hili ndilo jambo kubwa katika yote . Kumbuka wakati ulikuwa unapaswa kufanya kitu muhimu lakini ukatatizwa na hukuweza kukifanya? Ndio, hivyo ndivyo vikwazo hutokea . Ili kuikomesha dhidi ya kuiba ndoto zako, ziandike na uangalie maendeleo yako mara kwa mara. Shiriki ndoto zako na marafiki zako ili muweze kufanya kazi kwa pamoja na kusaidiana!
Kwa kuwa sasa unajua vitu vinavyoweza kuiba ndoto zako na jinsi ya kuvidhibiti unaweza sasa kuendelea bila kukoma katika safari ya ndoto zako!
Share your feedback