Wanawake na wasichana kote ulimweguni huboresha jamii, hii hapa ni namna wanavyofanya!
Wanawake hawa watatu waliboresha ulimwengu zaidi kwa ajili ya wasichana, kila mmoja kwa njia yake binafsi. Tunatumai maneno na vitendo vyao vitakuhamasisha kutaka kuboresha zaidi mji, kijiji, shule na nyumbani kwako.
"Fikiria kama malkia. Malkia haogopi kufeli. Kufeli ni jiwe jingine msingi la ukuu." – Oprah Winfrey
Oprah Winfrey ambaye alizaliwa na mama asiye na mume huko Mississippi kijijini nchini Marekani, alikuwa na hali ngumu utotoni. Lakini hakuruhusu umaskini kuwa kikwazo. Alijitahidi kwa kupiga hatua moja ndogo baada ya nyingine hadi alipokuwa mwendeshaji wa kipindi chake binafsi cha televisheni kilichoitwa, The Oprah Winfrey Show. Kilitokea kuwa mojawapo ya vipindi maarufu vya mazungumzo katika historia ya televisheni. Oprah ametumia ufanisi wake kusaidia kuboresha maisha ya wanawake wachanga wenye mahitaji na mojawapo ya njia hizo ni kupitia The Oprah Winfrey Leadership Academy for Girls Afrika Kusini. Kupitia miradi kama vile Leadership Academy anatumai kuelimisha na kuwezesha wasichana wachanga kote ulimwenguni ili baadaye wapige vita umaskini katika nchi zao.
"Ninafikiri wanawake zaidi wanapaswa kujihusisha na siasa kwa manufaa ya binadamu." – Aung San Suu Kyi
Aung San Suu Kyi ni mwanasiasa, mwandishi na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kutoka Mynamari huko Asia ya Kusini Mashariki. Alipewa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 1991 kwa ajili ya maandamano yake ya amani na yasiyo na ghasia dhidi ya ukosefu wa haki. Mwaka wa 2016 alikuwa mshauri serikali ya Myanmari. Aung San Suu Kyi amedhamiria kuhimiza wanawake wengine na wasichana kushiriki katika siasa na kutetea haki za wanawake. Anasema: “Lazima tuwafunze wavulana wetu sheria za usawa na heshima. Na lazima tuwafunze wasichana wetu kuwa wanaweza kufika kileleni kwa njia zote zinazowezekana.”
“Ni mambo madogo ambayo raia hufanya. Hilo ndilo litakaloleta utofauti. Jambo langu dogo ni kupanda miti.” – Wangari Maathai
Wangari Maathai ni mwanaharakati wa mazingira kutoka Kenya ambaye alizaliwa kijijini na akawa mwanamke wa kwanza wa Afrika kupokea Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 2004. Alianzisha Vuguvugu la Green Belt kama njia ya kuwaelimisha watu kuhusu manufaa ya kupanda miti. Aliamini kuwa hata vitendo vidogo zaidi kutoka kwa wanawake na wasichana vingesaidia kuboresha ulimwengu zaidi kwa ajili ya watoto wao na watoto wa watoto wao.
Share your feedback