Unaweza kujificha kwa jina la skrini, lakini tabia bado ni muhimu
Intaneti ni eneo bora la kuwasiliana na kujifunza kutoka kwa watu wa aina zote, lakini kumbuka: bado kuna mtu mwingine upande mwingine wa kompyuta — kama wewe tu.
Tabia ya kistaarabu inatumika kila mahali, ikiwemo kwenye Intaneti. Chukua jukumu la kuunda mazingira salama na ya furaha mtandaoni kwa kila mmoja kwa kuwa raia (Intaneti + raia), kuanza kwa vidokezo vya Mawasiliano sahihi mtandaoni (Intaneti + tabia ya kistaarabu).
“Jina Lako ni Nani?”
Kwenye mitandao ya jamii na majukwaa, huenda rafiki yako wa dhati akajulikana kama ‘KewlGirl2002’, lakini katika dunia halisi, labda ni Ani au Lisa au Miriam. Wasichana wengine hutambua ubunifu wao wanapoingia mtandaoni, na mtu mwenye soni kabisa huenda akawa mtu mwenye kupiga gumzo sana ambaye hujawahi kukutana naye.
Kumbuka: kuwa mwangalifu kwa maelezo yako ya binafsi! Huwezi kujua mtu anaye nyuma ya skrini ile nyingine, kwa hivyo usishiriki picha na maelezo ya binafsi na watu usiowajua. Kama ilivyo katika dunia halisi, asilimia 99 ya watu ni wazuri na wa kawaida — lakini hilo halimaanishi usijaribu kujilinda!
Pia kuwa mzuri. Mtu wako wa mtandaoni anaweza kuwa tofauti kabisa na wewe, lakini usiwahi kumwambia mtu kitu ambacho huwezi kusema ana kwa ana.
“NIMEKASIRIKA SANA!"
Wakati mwingine watu watakuwa wajeuri na wabinafsi kwenye Intaneti. Usiruhusu wakufikie. Kutumia lugha chafu na nzito mtandaoni si bora kuliko kuitumia katika maisha halisi. Ujumbe wa mtandaoni kwa herufi kubw wenye alama hisi unamaanisha kuwa unapiga kelele na kwamba unakasirika sana wakati wote. Hutampigia mtu kelele shuleni, basi usifanye hivyo kwenye Intaneti.
Lakini unapaswa kufanya nini ukijikuta kwenye majibizano ya mtandaoni? Chukua muda kupumua kwa ndani na utulie. Fikiria kuhusu jinsi ambavyo ungalijibu ungalikuwa ukizungumza na mtu huyo katika maisha halisi badala ya mtandaoni.
Mwandishi wa habari Najwa Shihab ni mfano bora kuhusu jinsi ya kushughulikia makabiliano ya dijitali. Akiwa mwandishi wa habari, ni mtu mashuhuri kwa umma na kuna watu wasiokubaliana naye — na watu hao hawawi wazuri kuhusu jambo. Hata watu wanapomtumia maoni ya kutisha kwenye Twitter, haanzi kuwatusi na kuwashambulia. Hata ana ujasiri wa kupuuza watu wengi wanaomshambulia mtandaoni. Ni mfano bora kwa wasichana kila mahali kuhusu jinsi unavyopaswa kuwa ili kutoa maoni yako na wakati wa kusahau — kwa sababu wakati mwingine wenye chuki watachukia, na wewe si wa kiwango hicho, sivyo?
Share your feedback