Sababu yangu kufanya mambo yanayonitisha

Na sasabu kwa nini hata wewe unapaswa kufanya hivyo!

Inaweza kuonekana ngumu, lakini napenda kujaribu angalau jambo moja ambalo hunitisha kila wiki. Kwa kukabiliana na hofu yangu nimekuwa na uwezo wa kufikia malengo na ndoto ambazo sikuwahi kufikiria zinawezekana.

Kuanzia kujifunza jinsi ya kuwa na ujasiri kwa kuinua mkono wangu juu katika darasa hadi kuanzisha duka ndogo la mapambo katika soko. Malengo haya yote yalianza kutokana na kufanya kitendo kidogo kinachonitisha na hatimaye ikawa kawaida na rahisi.

Haya ndiyo niliyojifunza nilipokuwa nikikabiliana na wasiwasi wangu na kutumia hofu yangu ili kunipa motisha wa kufiikia malengo yangu!

  1. Chukua muda kutambua sehemu ambapo hofu au usumbufu uko katika mwili wako. Ikiwa ni hofu ya kuongea mbele ya umma unaweza kuhisi wasiwasi au tumbo joto. Ikiwa ni kumwomba mtu kwa ajili ya miadi ya kuwa pamoja unaweza kuwa na hisa kali moyoni. Unapohisi jambo katika sehemu ya mwili wako, pumzika kwa muda. Pumua ndani na nje mara 5 kwa urefu, na kuzingatia sehemu ya mwili wako ambapo unahisi hofu. Kwa njia hii unapata kupumua ndani ushupavu katika mwili wako! Pia kumbuka kwamba hofu ni wazo tu kuhusu jambo folani la baadaye ambalo bado halijatokea. Kwa hiyo badala ya kufikiria itakuwaje nikishindwa, Fikiria ITAKUWAJE NIKIFAULU!
  2. Tambua mambo yanayokupa usaidizi. Hatua ya kujaribu jambo ambalo hujawahi kufanya inaweza kutisha sana hususan kama hauna usaidizi kutoka kwa mtu aliye na uzoefu wa jambo hilo. Pata mtu unayemuenzi au anayeelewa vizuri jambo unalotaka kujaribu na umwombe ushauri. Mara nyingi watapendezwa na kufurahia kushiriki vidokezo vyao pamoja nawe.
  3. Jipongeze sana na uwe na wakati kufanya jambo la kusherehekea. Bila kujali ni nini, hakikisha umekuwa na muda wa kusherehekea ujasiri wako. Ni rahisi sana kutofanya jambo ambalo linakupa wasiwasi - hivyo unapofaolu kufanya jambo ambalo linakutisha basi unapaswa kusherehekea! Pia - zawadi ya mwisho ni kwamba utachochea hisia chanya wakati unapotaka kujaribu jambo lingine la kutisha baadaye.

Je, ni jambo gani ambalo umekuwa ukitaka kujaribu lakini unaogopa sana? Jaribu hatua hizi na zitakufikisha mbali!

Share your feedback