Una tatizo la kusinzia kwenye dawati? Mbinu hizi za afya zinaweza kusaidia
Unapambana kumakinika shuleni? Au kope zako kuwa nzito zaidi na kutanabahi, mwalimu anakuomba uamke? Labda ni wakati wa kufanya mabadiliko kwenye baadhi ya tabia zako za kila siku ili ufaidike zaidi ukiwa shuleni!
Kifunguakinywa cha ubongo
Bila shaka unataka kulala kwa dakika nyingi, lakini kifunguakinywa ni muhimu kuliko dakika chache za ziada za kulala. Ili uwe na mwanzo mzuri wa siku yako, unahitaji kifunguakinywa kilichojaa virutubisho vitakavyokupa nguvu. Fikiria uji, nafaka au nafaka isiyosindikwa/mkate wa hudhurungi kwa siagi ya karanga, maziwa na kipande cha tunda. Kifunguakinywa bora kitahakikisha kuwa unakaa wima na kusikiliza darasani.
Usiwe na kiu
Mwili wako unahitaji maji safi ili kuweza kulisha seli za ubongo wako. Usipokunywa maji ya kutosha utakuwa mchovu na kutoweza kusoma. Si bora ikiwa unataka kufanya vyema darasani! Epuka soda au vinywaji vingine vyenye sukari na unywe maji – tafuta chupa kubwa ya plastiki, ambayo unaweza kujaza maji. Ubongo wako utakushukuru.
Kumbuka hili
Kumbukumbu nzuri ni muhimu ikiwa unataka kujifunza. Njia bora ya kulisha kumbukumbu yako ni kwa kirutubisho kinachoitwa iron. Unapata iron zaidi katika nyama nyekundu, nafaka isiyosindikwa/mkate wa hudhurungi, maharage, spinachi na karanga. Ikiwa unataka kuwa na kumbukumbu bora darasani, hakikisha umevila vyakula hivi.
Samaki ni muhimu
Aina nyingi za samaki zina mafuta ambayo ni muhimu sana kwa ukuaji wa ubongo. Mafuta haya huhakikisha kuwa seli za ubongo wako zimebeba ujumbe wa kumbukumbu. Unapaswa kujaribu kula samaki angalau mara mbili kwa wiki. Ikiwa hupendi hivyo au huwezi kupata samaki unapoishi, samaki wa mkebe pia ni watamu na bora kwa afya. Vinginevyo unaweza pia kupata nyongeza hizo za kumbukumbu katika maziwa, jibini na mayai.
Share your feedback