Vidokezo rahisi vya kula vizuri
Wengi wetu hatushughuliki na kile kilicho kwenye sahani, tunajua tu tunakipenda au hatukipendi. Lakini tunakula chakula sio tu kwa sababu tunahisi njaa au kwa sababu kina ladha tamu, tunakula pia ili tupate virutubisho vinavyofaa ambavyo akili na mili yetu inahitaji ili kuendelea kuwa thabiti na kuepuka ugonjwa.
Kutafakari cha kula na kujua vyakula vinavyofaa mara nyingi huchanganya, lakini haifai kuwa hivyo. Hatua ya kwanza ni kuelewa aina tofauti za vyakula na jinsi husaidia mwili wako kua na kuwa thabiti.
Kuna aina tano za vyakula...
Mboga
Hii inapaswa kuwa sehemu kubwa kwenye sahani yako. Mboga zimejaa vitamini na madini ambayo husaidia mwili wako kukua na kuwa thabiti, lakini pia zimejaa ufumwele (fiber) ambao husaidia kushiba.
Matunda
Tunda limejaa vitamini na madini. Kula rangi na aina nyingi unavyoweza. Lakini usidhani kuwa kunywa sharubati ya tunda kutafanya kazi ya tunda, huenda imejaa sugari (lakini bila virutubisho bora) usiyohitaji.
Nafaka
Nafaka zinapaswa kuwa robo ya mlo wako. Mahindi, wali, mikate, na viazi ni vitamu, vilivyojaa ufumwele na bila shaka vitakushibisha. Jaribu kula nafaka za hudhurungi kama unaweza, chakula kilicho na nafaka za hudhurungi zina ufumwele na virutubisho vingi kuliko zile nyeupe au zilizosindikwa (processed). Na ukumbuke, jaribu kuepuka nafaka zilizopikwa kwa sukari, chumvi na mafute mengi kama keki au vibanzi vya viazi.
Protini
Protini imejaa virutubisho ambavyo mwili unahitaji ili kuwa thabiti. Huna uhakika ni chakula kipi cha protini? Fikiria nyama ya ng`ombe, kuku, maharage, dengu, karanga na mayai. Ukimsikia mtu akizungumza kuhusu 'chakula cha akili', anazungumzia protini!
Maziwa
Maziwa yamejaa kalsiamu ambayo ni sawa na chakula cha mifupa na meno yako. Na hupatikana katika maziwa, gururu (yoghurt) na jibini (cheese) tamu.
Kwa hivyo ni vipi unayvosawazisha ni vyakula vipi unavyopaswa kula, wakati gani na kiasi gani? Mlo wenye afya unapaswa kuwa na vyakula vyote kutoka kwenye vikundi tofauti vya vyakula. Si lazima viwe vigumu – unachohitaji kufahamu ni vidokezo hivi rahisi 5 vya mlo.
1. Nusu/nusu: Nusu ya sahani yako inapaswa kuwa tunda na mboga. Kumbuka, mboga na matunda tofauti yana virutubisho tofauti na husaidia mwili wako kwa njia tofauti. Hivyo jaribu kuibadilisha mara nyingi uwezavyo. 2. Nafaka ya nishati: Ni robo moja tu ya sahani yako inayopaswa kuwa na nafaka zenye afya. 3. Zilizo na protini: Robo ya sahani yako inapaswa kuwa na protini yenye afya. 4. Maziwa hayatishi: Kunywa maziwa au maji mengi badala ya vinywaji vyenye gesi au sukari. 5. Usizidishe: Chakula ni jinsi tunavyoirutubisha mili yetu kuwa thabiti na bila ugonjwa. Hivyo jaribu kuepuka kula viwango vikubwa wakati usipovihitaji. Usikilize mwili wako unapokuwa umeshiba. Ni sawa kuacha kula.
Share your feedback