Jinsi nilivyomwambia baba yangu kuhusu hedhi yangu!

Haikuwa mbaya kama nilivyofikiri itakuwa

Nilipopata hedhi yangu kwa mara ya kwanza, sikushtuka wala kuogopa, kwa sababu katika kundi langu la marafiki tulikuwa tumezungumza mengi kuhusu hedhi, na rafiki yangu mmoja au wawili walikuwa wameshapata hedhi zao miezi michache kabla.

Nilichohofia ni kulazimika kumwambia baba yangu!

Nyumbani, yupo baba yangu, mimi na dada yangu mdogo tu. Wakati mwingine ni vigumu kueleza kwake “mambo ya wasichana” kwa sababu hajapitia mambo haya. Lakini kwa hili, nilijua ilibidi tulizungumzie.

Niliandika mapema jinsi nitakavyomwambia. Najua anafahamu jinsi hedhi huwa, lakini nilitaka ajue kwamba ilikuwa wakati wa muhimu sana katika maisha yangu, na kwamba kwa sababu hatuna mama ningehitaji msaada kutoka kwake kununua pedi za hedhi na pengine dawa za kupunguza maumivu kama ningeteseka na maumivu ya tumbo au kichwa.

Baada ya chajio jioni moja, dada yangu alipokuwa ameenda kulala, nilivuta pumzi kubwa na kumwuliza baba yangu kama tungeweza kuzungumza. Moyo wangu ulikuwa unaenda mbio, lakini nilipomwambia, uso wake uliyasema yote. Alijivunia sana mimi kuwa jasiri vya kutosha kuzungumza naye kuhusu hilo na akasema kwamba atakuwapo kwa ajili yangu ikiwa nahitaji chochote au nina maswali yoyote, na kwamba hakuna chochote cha kuonea aibu ninapotaka kumwomba.

Nilihisi nimetulia! Hatua hii kubwa katika maisha yangu ingekuwa wakati mgumu, lakini baba yangu alikuwa na utulivu nayo. Na sasa nafahamu kwamba nina msaada wake, ninafuraha sana.

Kwa hivyo kama unahitaji kuzungumza na mzazi au mlezi kuhusu hedhi yako, au mada nyingine ambayo una wasiwasi au aibu juu yake, jaribu vidokezo hivi:

  1. Kuwa na ujasiri (hata kama hauhisi jasiri kwa ndani!)
  2. Kuwa mtolivu na usiwe na aibu – hedhi ni ukweli wa maisha wa binadamu.
  3. Itisha msaada ikiwa unahitaji.
  4. Elezea waziwazi hisia zako.

Unaweza!

Share your feedback