Jinsi nilivyotoka katika hali mbaya
Niliposimama kutoka kwa kiti changu cha shule na nikaona mpakato wa damu juu yake – uso wangu uligeuka mwekundu kama ile damu! Nilifahamu kwamba ilikuwa imeshuka kupitia sketi yangu. Niliketi chini tena, bila uhakika wa nitakacho fanya baadaye.
Hedhi yako ya kwanza haikuji unapoitarajia. Kwangu, ilikuwa katikati ya kipindi cha Bi. Moonie cha hesabu.
Nilipitisha dokezo kwa rafiki yangu wa dhati Amie ambaye alikuwa viti viwili kando yangu. Amie alingoja nami hadi kipindi kikaisha, kisha akamwambia Bi. Moonie kilichokuwa kinaendelea. Waliweza kunipeleka msalani ambako niliweza kujisafisha. Bi. Moonie alinitafutia pia sketi ya kuvaa.
Nilimpigia mama simu kumwambia ile habari. Nilikuwa na wasiwasi –ingawaje tulikuwa tumeizungumzia kabla. Alikuwa na msisimko sana, na hata alisema “hongera”! Alikuwa na dada yangu mkubwa ambaye alifurahi pia. Majibu yao yalinifanya nipunguze wasiwasi, na nilihisi kwamba wangenisaidia kwa kile nilihitaji kusimamia hedhi zangu.
Baada ya muda wa shule, Amie alipanga wasichana kadhaa kuja nyumbani. Tulipokula keki ambayo mama alileta, wasichana kadhaa walianza kuniambia hadithi zao za hedhi.
Hadithi ya Sara ndiyo nilikuwa na wasiwasi nayo. Hedhi yake ilianza katika kipindi cha kuogelea. Lakini mwalimu wake aliona na akasaidia kuwavuruga wanafunzi wengine na kumtoa kutoka katika hali hiyo bila hangaiko.
Wiki chache zilizopita, Hanna alishtuka wakati pedi ilipoanguka kutoka kwenye mkoba wake wa michezo mbele ya mpenzi wake Tim. Lakini Tim alichukua pedi ile, akampa na akatabasamu tu. Kisha wakaenda kwa darasa lao pamoja na kuzungumzia jambo lingine – hakuna ubaya wowote.
Baada ya mchana wa kubadilishana hadithi za hedhi, nilihisi kuwa jasiri zaidi kukubali sura hii mpya katika maisha yangu. Sitaepuka shule, kuogelea au kujihusisha kwa sababu ya hofu yoyote kuhusu hedhi yangu. Hakuna kitu cha kuona aibu! Hata nikikwama katika hali mbaya – marafiki zangu, walimu na wazazi wanaweza daima kunisaidia.
Share your feedback