Viungo vyaVisodo

Utahitaji kimoja kwa siku kadhaa kila mwezi

Labda umekiona kwenye mfuko wa dada au mama yako na ukashangaa ni cha nini. Basi, kinaitwa Kisodo!

Wakati utawadia ambapo mwili wako utapitia mabadiliko. Hii inaitwa ubalehe na hii inakuja na kuanza kwa kupata hedhi. Tunatumia visodo wakati wa hedhi. Kabla ya kupitia jinsi ya kuvitumia turejelee kinachotendeka wakati wa hedhi.

Wakati wa hedhi ni sehemu ya tunachokiita mzunguko wa hedhi, jambo linalotokea kila mwezi kutayarisha miili yetu kupata mimba. Inaenda hivi:

Day_1-7_CveOcif.png

1). Siku 1-7: mzunguko wa hedhi huanza ambapo tumbo letu la uzazi linatoa bitana ya chupa ya mtoto. Mwili wako hutoa hii kama damu kupitia uke wako. Hii inaitwa hedhi na inatendeka kwa siku kadhaa, kulingana na kila mwanamke. Hapa ndipo tunatumia visodo kunyonya ile damu.

Day_7-14_6qzbmJn.png

2). Siku 7-14: Hapa ndipo mfumo wa kutokeza yai huanza. Ovari zako hujitayarisha kutengeneza yai. Kwa wakati huu, tumbo lako la uzazi pia huanza kuunda bitana mpya yachupa ya mtoto.

Day_14-17_2mL1dFH.png

3). Siku 14-17: Hapa, ovari zako zinawachilia lile yai na linaenda hadi kwenye tumbo lako la uzazi. Huu ni wakati ambapo unaweza kushika mimba haraka sana. Tumia mbinu za kupanga uzazi unapofanya ngono kama hauko tayari kupata mimba - na kuzuia magonjwa ya zinaa.

Day_17-25_AjaTt2o.png

4). Siku 17-25: Yai huendelea kutembea katika tumbo la uzazi. Kama halitakuwa halitatungishwa, litavunjika na kutolewa mwilini.

Day_25_aN98H7b.png

5). Siku ya 25: Mwili wako utatoa bitana ya chupa ya mtoto kutoka kwenye tumbo lako la uzazi na mzunguko wa hedhi utaanza upya.

Maajabu? Hivyo ndivyo hedhi huwa. Hata hivyo sio mzunguko wa hedhi wa kila mtu utafuata muundo huu. Hedhi hazifuati muundo mmoja unapoanza na hii ni kawaida.

Sasa tunajua visodo ni vya kazi gani. Hivi ni baadhi ya vidokezo unapotumia kisodo:

New_napkin_BhbOR8r.png

a). Hakikisha kisodo ni kipya na kimefungwa, ili kuhakikisha ni salama na safi.

Remove_strips.png

b). Toa ile sehemu ya plastiki ya kisodo kabla ya kukiweka juu ya chupi yako, ili kutumia gundi iliyo nyuma yake. Gundi ile huweka kisodo salama kwenye chupi yako. Bila hivyo kinaweza kusonga au kuanguka.

c). Kuna visodo vya aina kadhaa, kulingana na bajeti yako na mahitaji. Chagua kinachokutosha vizuri.

Change_napkin_HdmCPjK.png

d). Badilisha kisodo kinapojaa au baada ya masaa sita. Kitupe vizuri ili uwe safi kila wakati!

Share your feedback