Nini kinaendelea juu ya hedhi yangu?

Mwili wako unajirekebisha!

Huenda unashaanga mbona hedhi yako inaonekana kuchelewa miezi kadhaa, na mapema kwa miezi mingine, na wakati mwingine haiji kabisa. Hedhi isiyo fuatana ni kawaida kabisa mwanzoni. Mwili wako unajifunza jinsi ya kudhibiti mzunguko wako na inaweza kuwa miezi au hata miaka, kabla ya kuwa na hedhi za kawaida.

Kuna sababu zingine kwa nini hedhi yako isiwe ya kawaida – unaweza kuwa umekonda sana, mnene sana, na mwenye mafadhaiko mengi, au hauna madini ya chuma ya kutosha kwenye damu yako. Ikiwa hedhi yako haikuja kabisa, hii ni mwili wako unakutumia ujumbe. Kukaa kwa afya ni muhimu, hivyo hakikisha unakula vyakula vilivyo na protini (kama kuku, mayai na karanga) na pata usingizi wa kutosha.

Njia bora ya kufuatilia hedhi yako ni kuhesabu mzunguko wako, ili uweze kufahamu wakati wa kutarajia hedhi yako. Ikiwa ni mzunguko wa siku 28, hedhi yako inapaswa kudumu siku 5 hadi 7. Hivyo hesabu kutoka siku ya mwisho ya hedhi yako iliyopita na wacha kuhesabu siku ya kwanza ya hedhi ijayo. Fanya hivi kwa miezi mitatu na kama idadi ya siku kati ya kuwacha na kuanza hedhi ni tofauti sana kila mwezi, inamaanisha mzunguko wako sio wa kawaida.

Wasichana wengine hawana usawa wa homoni unaosababishwa na sababu za mtindo wa maisha (mazoezi mengi au lishe, mafadhaiko au kumeza kidonge cha kupanga uzazi) au hali ya matibabu (kama polycystic ovarian syndrome), na hii inaweza kuwa ndio sababu ya hedhi zisizo za kawaida pia.

Ni muhimu kuanza kutunza mwili wako. Kujitunza mwenyewe kutakuwezesha kusimamia viwango vyako vya mafadhaiko, kiasi kizuri cha mazoezi kitakuweka vyema na kuzalisha homoni za kujisikia vizuri, na kula vyakula vya afya kutahakikisha unaupatia mwili wako nguvu inayohitaji kufanya kazi vizuri.

Ikiwa hutapata hedhi yako kwa miezi michache au ikiwa itachukua muda mrefu Zaidi ya siku 7, basi unashauriwa kwenda kumwona daktari wako au zungumza na mtu mzima ambaye unaamini na unajisikia vizuri kuongea naye.

Share your feedback