Joanna aliuzwa kwa ajili ya hela

Sasa ana ujuzi wa kupata hela zake

Tulipounda Azimio la Msichana, zaidi ya wasichana wachanga 500 walihojiwa kwenye nchi zote 14. Kisa cha Joanna kinaakisi changamoto zinazowakabili wasichana wengi tuliozungumza nao...

Usalama wa Kiuchumi

Kisa cha Joanna ni mfano wa kwa nini lengo la 4 la Azimio la Msichana - usalama wa kiuchumi - ni muhimu sana.

Kama msichana mchanga familia yake ilimwuza kwa sababu ilihitaji hela za ziada. Walimwona kama mzigo kwenye fedha zao.

Lakini Joanna alipowatoroka watu waliomnunua, na alipopewa fursa ya kujifunza ujuzi mpya ambao ungemwezesha kujikimu - kama vile kukuza chakula ambacho anaweza kuuza - alinawiri na kuwa mwanamke mchanga wa kujitegemea ambaye angeweza kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi wa jamii yake miaka mingi ijayo.

"Ni muhimu kwa wanawake nchini Liberia kuwa na biashara yao binafsi," anasema. "Kwa sababu ukiwa na biashara yako binafsi, hakuna mtu anayeweza kukuhangaisha."

Share your feedback