Hadithi za uongo 3 kuhusu wavulana!

Wavulana hubalehe pia!

Ubalehe ni jambo ambalo tunapitia sote. Inaweza kuwa safari yenye changamoto sana na mara nyingi unahisi kama unaipitia pekee yako, lakini haufai kuhisi hivi!

Kuzungumza kuhusu mambo kama hedhi na mihemko ya hisia na watu waliokaribu nawe inaweza kukusaidia kupata maelezo zaidi kuhusu mabadiliko unayopitia. Ni mbinu nzuri pia kupeana na kupata ushauri.

Wakati mwingine tunahisi ugumu kuzungumza na wavulana kuhusu ubalehe kuliko tunavyohisi tunapozungumza na wasichana, mara nyingi kwa sababu tuna wazo lisilofaa kuhusu wanavyotufikiria.

Basi Spingsters, tuko hapa kuzungumzia hadithi hizo za uongo!

Hadithi 1 - Miili ya wavulana haipitii mabadiliko

Kwa sababu wavulana hawana hedhi haimaniishi hawapati kubalehe pia. Kama sisi tu, miili yao pia inapitia mabadiliko na marekebisho! Kwa mfano, Je, ulijua huu ni wakati ambapo wavulana huanza kumea nywele kila mahali na sauti zao zinakuwa nzito?

Hadithi 2 - Wavulana hawajui chochote kuhusu wasichana

Hii si kweli, lakini kama una rafiki au ndugu wa kiume ambao hawaelewi unachokipitia, waambie! Jitayarishe kwani huenda wakawa na maswali mengi sana - jibu tu ambayo uko sawa nayo!

Hadithi 3 - Wavulana hawajali kuhusu tunachokipitia

Wavulana wanaweza kuwa wasikilizaji wazuri sana na wanavutiwa sana na wema wetu kuliko tunavyofikiri. Hata kama wakati mwingine hauhisi hivyo, wanajali kuhusu tunayoyapitia.

Ubalehe unaweza kuwa wakati mgumu sana, lakini kadiri tunavyozungumza wazi wazi kuuhusu, ndivyo marafiki wetu wa karibu wanatuelewa.

Kuwa mkweli na wazi miongoni mwetu kutatusaidia kupata taarifa zaidi. Ubalehe sio jambo la kuogopa, tunapitia sote!

Share your feedback