Kuwa Miss Independent – Sehemu ya 2

Usiwache hadi Umalize

Vipi dada,

Wakumbuka nilivyokuambia kwenye hadithi yangu iliyopita Kuwa Miss Independent – Sehemu ya 1 kunaanza na kujiamini? Kama hujaisoma bado, nenda hadi chini ya ukurasa huu na ubofye kwenye sehemu ya “Unaweza Penda.”

Hata hivyo, ni kweli kabisa kwamba kujiamini ni muhimu. Tangu nianze kuwa na mtazamo mzuri wa maisha, mambo mazuri yamekuwa yakinitendekea.

Kama lile wazo nzuri la biashara nililopata mwezi uliopita. Mimi na nyanya yangu daima tulipenda kuoka keki pamoja na kila wakati watu walipotutembelea wangeuliza kuhusu keki zetu. Kwa hivyo nikawaza, mbona tusianze kuuza keki ili mtaa mzima uweze kununua.

Lilitokea kama wazo rahisi mwanzoni, lakini kuanzisha biashara yako mwenyewe sio jambo rahisi hata kidogo. Kuna mambo mengi ya kuzingatia na mambo mengi zaidi yanaweza kwenda mrama. Lakini nikakumbuka, usizingatie mambo mabaya. Ili kujitegemea lazima uamini kwamba licha ya yanayotendeka maishani mwako, una nguvu kuyashinda na unaweza simama wakati wowote.

Nilitaka kuanza kuuza keki kwenye soko la mtaani kabla sijapata kibanda changu mwenyewe ili nipime mapishi. Kwa hivyo nilienda kwa muuzaji wa mikate mtaani na nikamuuliza kama ninaweza kuuza keki zetu kwenye kibanda chake. Alikubali na akanipa pesa ninunue viungo vyangu vya kwanza. Nilikuwa na msisimko sana. Nilikuwa nimepiga hatua moja kuwa huru.

Nilipokuwa nikirudi nyumbani nianze kuoka keki, pikipiki niliyokuwa nimekalia ilisimama ghafla. Niliyumbishwa na viungo vyangu vyote vikaanguka sakafuni. Nilifadhaika sana! Nilikuwa nimeahidi mwokaji yule kwamba ningempelekea keki siku iliyofuata lakini sasa sikuwa na viungo wala pesa za kununua vingine. Sikujua nifanye nini. Nilitaka tu kukata tamaa. Mbona maisha ni magumu hivi?

Nilipokuwa nimesimama pale nikiangalia ndoto zangu za kujitegemea zilivyotapakaa pale sakafuni, nilisikia sauti ya nyanya yangu kichwani. “Mawazo hasi hayatakupa maisha mazuri.” Kwa hivyo niliyaondoa mawazo haya kichwani na nikaanza kujiambia kuwa kila kitu kitakuwa sawa. Wakati ule niliamua sitakata tamaa na nitakuwa imara.

Haya yote yalinifunza kuwa safari ya kujitegemea sio barabara nyoofu. Ina panda shuka lakini jambo la muhimu ni kuendelea kusonga mbele.

Ungependa kujua nilivyosimama tena? Soma sehemu ya 3 hapa chini ili ujue…

Share your feedback