Usifanye safari hii pekee yako
Vipi dada,
Nimekuwa nikishiriki safari yangu ya kuwa Miss Independent. Sina uhakika kama umeona hadithi zangu zingine, lakini nimekuwa nikipanga kuanza biashara ya kuoka keki nilipopata msiba! Nenda hadi chini kwenye sehemu ya “Unaweza Penda” ili usome sehemu ya 2 upate kujua kilichotendeka.
Baada ya tatizo nililopata, sikuwa nikate tamaa kwa sababu nilijiamini na nilikuwa na mawazo mazuri kuhusu matokeo. Badala ya kukata tamaa niliamua kuwa na raha kiasi na nikajipiga picha kando ya viungo vyangu vyote pale sakafuni na nikaweka kwenye mtandao wa kijamii. Maelezo yangu mafupi yalisema – “Ninahitaji kuoka keki 50 ifikapo kesho lakini sina viungo #tumausaidizi”.
Nilipokuwa nafika nyumbani, nilikuwa nimepokea jumbe nyingi sana kutoka kwa marafiki na majirani wakisema walikuwa na unga, siagi, maziwa na sukari zaidi! Ajabu kiasi gani? Kwa hivyo walikuja nyumbani kwangu kunipa viungo vile na kunisaidia nitayarishe kila kitu ili niweze kuuza siku iliyofuata.
Nikitafakari juu yake… ningefanya nini bila marafiki zangu? Niliishi kufikiria kuwa kujitegemea kulimaanisha ulihitajika kufanya kila kitu mwenyewe, lakini hiyo si kweli hata kidogo. Ushirikiano ni kitu cha muhimu na ni kiungo cha siri cha maisha. Kama nilivyoeleza mbeleni, safari ya kujitegemea ni ngumu; kwa hivyo unahitaji kuwa na marafiki wanaokupenda na kukusaidia kila wakati. Haufai kuhisi kama kwa kuomba msaada unakuwa mzigo kwa watu wengine. Haujapangiwa kupitia maisha pekee yako!
Kwa hivyo, unapoanza safari yako ya kujitegemea kumbuka:
1. Jipende na uamini mambo mazuri kujihusu.
2. Hata mambo yakiwa magumu… USIFE MOYO.
3. Usijaribu kufanya mambo yote peke yako. Tafuta usaidizi kwa marafiki na familia ukihitaji. Hii haimaanishi hujitegemei.
Mwishowe nilikuwa na keki zangu 50 tayari na nikafika kibandani kwa wakati ili niweze kuziuza. Nilitengeneza pesa zangu za kwanza na nilihisi vizuri. Ilinichukua muda kufika pale lakini nimejifunza mengi kunihusu na maana ya kujitegemea.
Share your feedback