Jinsi rafiki yangu alivyonisaidia kuimarisha ujasiri wangu
Jina langu ni Aarani na nimetoka Bangladeshi. Ninaishi katika eneo la Rangpur. Familia yangu na mimi tulikuwa tumehamia sehemu nyingine ya nchi kwa sababu hakukuwa na kazi katika mji wangu wa nyumbani. Nilipoanza shule kila mtu angeweza kujua mimi nilikuwa tofauti nao. Watu walinichekelea na wakaniita majna kwa sababu nilikuwa naonekana tofauti. Nilijihisi mpweke kwa sababu sikuwa na mtu wa kuongea na yeye. Nikaamua kumpigia simu rafiki yangu kutoka nyumbani, Barnini kumwelezea ni nini kilichokuwa kikiendelea. Akanikumbusha kuwa mimi ni wa maana. Akanisaidia kugundua uwezo wako wa kipekee na utu wangu wa kupendeza. Kama alivyofanya, niliweza kupata marafiki walionipenda na waliofaa urafiki wangu.
Alinifunza pia kwamba urembo hutoka ndani na hautegemei jinsi watu wengine wanavyonifikiria. Maneno yake yalinipa faraja niliyohitaji ili kukabiliana na wanyanyasaji shuleni.
Kwenye simu alinifunza zoezi nzuri sana la kuongezea ujasiri wangu. Nilitafuta karatasi na nikaandika mambo yote mabaya ambayo watu wamekuwa wakiyasema kunihusu shuleni. Nilipomaliza nilikunja karatasi hiyo na kuitupa kwenye takataka. #byehaters kisha nikatafuta karatasi nyingine na kwa pamoja na rafiki yangu nikaandika mambo yote mazuri kunihusu na nikaibeba kila mahali.
Sasa kila asubuhi au wakati wowote ninapohisi vibaya ninaisoma kwa sauti kwamba nina nguvu, mimi nina thamani, nina kipawa, mimi ni mtu mzuri sana! Kujiona hivi hunipa ujasiri ninaohitaji kukutana na watu wapya na kupata marafiki wa kweli.
Ningefanya nini bila rafiki yangu kweli? Ijapokuwa ako mbali sana bado alinifunza jinsi ya kujiamini na kuimarisha imani yangu. Urafiki ndio huo, lazima mjengane. Barnini amekuwa nguzo yangu kwa kila kitu na nitaendelea kumfurahisha kwa kufuata ushauri wake na kusema KWAHERI kwa mambo mabaya. Daima watu watakuwa na jambo la kusema lakini na marafiki wazuri karibuni na mimi ninachagua kuzingatia mambo mazuri!
Share your feedback