Bosi wa kike wa Miaka 17

Wazo rahisi lilibadilika kuwa kubwa

Jina langu ni Laurence na ninaishi katika mji mdogo ambao una biashara nyingi ndogo ndogo zinazojitegemea. Mfanyabiashara mmoja ambaye nimekuja kumfahamu vizuri ni Pat, ambaye nilikuwa nanunua mboga zetu zote kwake.

Miaka kadhaa iliyopita Pat aliniambia kwamba alikuwa na hofu kwa sababu msambazaji wake mkuu alikuwa anafunga biashara na hii ingeathiri biashara yake. Nilifahamu kwamba familia yake ilikuwa inategemea pato lake, kwa hiyo niliamua kuchukua hatua.

Nilianza kwa kuuliza wafanyabiashara wote mtaani kuhusu wasambazaji wao wakuu na punde nilikuwa na orodha ya wakulima wote wa eneo letu. Halafu nikamuuliza baba yangu kama ninaweza wapigia wakulima wale simu kuwauliza kama wanaweza nifunza ustadi uliohitajika kukuza mboga zangu mwenyewe. Baba yangu alinipa pointi kadhaa za jinsi ya kuzungumza na wakulima wale. Aliniambia nijieleze kwa nini ninataka ushauri wao, kwamba nilikuwa nafikiria kukuza na kuuza mboga zangu mwenyewe ili nimsaidie Pat na familia yangu vilevile. Mkulima mmoja alichukua muda kunifunza yote kuhusu kukuza mboga – aliniambia kwa nini kutumia udongo unaofaa ni muhimu, mbinu sahihi za kupanda jinsi ya kudhibiti wadudu na wakati wa kuvuna. Nilianza kidogo na nikamwambia Pat kuhusu biashara yangu mpya na kwamba niliomba iwe kubwa ili labda niwe msambazaji wake mkuu!

Mara ya kwanza nilikuwa na mboga kiasi tu za familia yetu kutumia na za kuuzia marafiki, lakini punde shamba langu lilianza kustawi na neno likasambaa. Hii ilinipa fursa ya kuanza kuziuzia biashara ndogo ndogo, kama ya Pat, ili waweze kuendelea kuuza.

Jambo bora ni kwamba Pat ana tajriba ya miaka mingi katika biashara kwa hiyo aliketi chini na kunipa ushauri jinsi ya kutunza biashara yangu mpya, ikiwa ni pamoja na fedha na akiba. Hata sikuwa nimewaza kuhusu baadhi ya mambo hayo, kwa hiyo nilishukuru sana kwa ushauri wake.

Leo, ninauza kwa biashara kadhaa ndogo ndogo ambazo zinawauzia watu wa mtaani katika mji wetu na sote tunafaidika na huu mfumo mpya.

Kwa hiyo, kama una wazo – liwe dogo au kubwa – chukua hatua ya kwanza ya kumuomba mtu msaada au ushauri. Kama unahisi uoga au aibu, jaribu kuandika lengo lako na jinsi unavyofikiri utaweza kulitimiza, halafu kabiliana na woga wako, vuta pumzi ili utulie na anza kuitimiza! Unaweza usifanikiwe na mtu wa kwanza utakayemuliza, lakini usife moyo. Sikudhani nitajifunza mengi kutoka kwa mkulima au kutoka kwa Pat, lakini nimejfunza kwamba sio lazima uangalie mbali ili kupata mshauri bora!

Share your feedback