Ushauri kutoka kwa rafiki yangu wa dhati wa kiume.
Nilipokuwa kijana wasichana wengine shuleni waliniambia kwamba wavulana ni wabaya na ni lazima nikae mbali nao. Walisema kwamba wavulana na wasichana hawawezi kuwa marafiki pamoja. Ningewasikiliza lakini moyoni nilijua sio kweli.
Nina rafiki wa dhati wa kiume anayeitwa Kofi. Tumekuwa marafiki tangu kuzaliwa. Mama zetu ni marafiki na tulizaliwa siku moja. Yeye amekuwa akinichukulia kawaida. Haikujalisha kama mimi ni msichana au la. Sisi sote tumependa mambo yanayofanana. Sisi sote tunapenda mpira wa miguu. Sote wawili tunapenda mboga zetu. Sisi sote tunapenda kusoma vichekesho. Ningeweza kuendelea.
Hata hivyo tulipoanza shule ya upili, kijana mwenye umri zaidi yangu alivutiwa na mimi. Alikuwa akijaribu daima kuzungumza nami kwenye korido lakini nilikuwa na aibu. Aliendelea kujaribu kuzungumza na mimi mpaka hatimaye nilipokubali. Tulipoanza kuzungumza mambo yalienda vizuri mpaka ghafla alipoacha kuzungumza nami. Siku iliyofuata nikamwona akitembea na msichana mwingine.
Nilihuzunika sana, nilidhalilika sana kana kwamba kuna kitu kibaya kwangu. Nilimwomba Kofi kwa ushauri kwa nitakachofanya maana alikuwa mvulana.
Kofi alinikumbusha kwamba hakuna kitu kibaya kwangu. Alisema dhamani yangu haikutegemea kama mvulana alinipenda au la. Dhamani yangu inatoka ndani yangu na hakuna anayeweza kuiondoa.
Pia aliniambia nisivunjike moyo. Iwapo mienendo ya mvulana haieleweki kwangu, haina uhusiano na mimi bali inahusiana na yeye mwenyewe na mashaka yake.
Sasa ninatambua jinsi gani mimi ni wa kipekee. Pia ninafahamu kuwa mvulana yeyote atakayenipenda ataniheshimu. Hatajaribu kuniaibsha au kutaka kuwahisha mambo. Ninawashukuru sana marafiki wa dhati wa kiume kama Kofi. Inathibitisha kwamba wavulana wanaweza kuwa marafiki wazuri na kukupa ushauri wa muhimu sana.
Share your feedback