Mfadhaiko unaudhi

Jina langu ni Ari. Wakati mwingine ninafadhaika. Kufadhaika si sawa na kuhuzunika. Ni huzuni nyingi ambayo inaweza kukufanya kuhisi kutokuwa na matumaini, kushindwa na kutokuwa na thamani. Kwa kawaida huwa kitu unachohisi kwa kipindi kirefu, sio tu siku moja au mbili. Wakati mwingine kuna sababu, wakati mwingine haieleweki ni kwa nini unahisi hivyo. Pia kuongezea kwenye hali, wakati fulani katika maisha yetu tunakumbana na mabadiliko mengi na viwango vya homoni za ajabu. Mfadhaiko unaudhi. Mfadhaiko unakushusha chini zaidi. Huenda usiwe na hamu ya kula, kulia bila sababu kabisa, au kwa ghafla hufurahi vitu vyote unavyopenda kuvifanya. Unaweza kukasirikia maisha yako na kitendo kidogo tu cha kuondoka kitandani huenda kikaonekana kama kazi ngumu sana. Umewahi kushuhudia hali hii? Usijali. Ni Sawa kabisa kutokuwa Sawa.
Kitu cha kwanza unachohitaji kufahamu ni kwamba ni kawaida kutamauka wakati mwingine. Wewe si wazimu. Chukua muda wako na usijali kuhusu muda ambao umekuwa ukihisi hivi. Ni tofauti kwa kila mtu.

Lakini tahadhari, wakati mwingine ushauri wa marafiki na wanafamilia wasioelewa unachohisi, unaweza kukuacha kuhisi kukasirishwa zaidi au kuhuzunika zaidi. Mama yangu anaponiambia ‘changamka!’ anataka kusaidia. Hakusudii kuongeza mfadhaiko wangu. Lakini labda hajui unachohitaji. Intaneti ni zana bora sana ikiwa unatafuta taarifa zaidi kuhusu mfadhaiko au kupata wengine walio na hali kama yako kabisa.

Ukijipata huna matumaini siku nyingi, kuchoka mara kwa mara, kupoteza mvuto wa vitu vingi ambavyo hufurahia na kufikiria sana kuhusu kifo au kujitia kitanzi, huenda ukahitaji kutafuta usaidizi. Zungumza na mtu unayemwamini, mwalimu wako, na wazazi wako kuhusu hisia zako. Fahamu ikiwa kuna mshauri unayeweza kuzungumza naye kwenye kliniki yako ya karibu au ikiwa kuna simu ya usaidizi unayoweza kupiga.

Kumbuka kuwa si wewe pekee yako, kuna watu wanaokujali. Mamilioni na mamilioni ya wasichana wapo hapa nasi. Na inauma, lakini hatuko peke yetu.

Share your feedback