Bado unaweza kutimiza ndoto zako.
Nilipokua nilipata ugumu kusoma sababu nilipokuwa na miaka 5 nilipata ajali ya gari iliyonisababishia majeraha ya ubongo.
Madaktari walisema sitakuwa kama awali tena. Baadhi pia walisema sitaweza kukabili vitu vingi maishani sababu ya ulemavu, lakini sikuwaamini.
Bibi yangu daima alinambia kuwa mimi ni wa kipekee na nisiruhusu ulimwengu uniwekee mipaka. Hivyo nilifanya maamuzi kumsikiliza na nilipuuza maneno yote ya kunipinga.
Ingawaje nilikumbana na ugumu kusoma darasani, niligundua kwamba nilikuwa na ujuzi wa kutengeneza vitu. Historia na Jiografia yaweza kuwa hayakuwa masomo ninayoyamudu, lakini nipe redio na ningeweza kuitengeneza! Nipe gari na ningeweza kufanya injini ifanye kazi tena!
Niliwaambia wazazi wangu kuhusu ndoto zangu kumiliki duka la kurekebisha magari siku moja na wakaipenda! Baba yangu alipendekeza nianze kidogo wangu kwenye gereji yake. Punde kila mtu alinijua kama fundi na biashara kidogo kwa kusaidia watu kwenye jamii yangu na kufanya pamoja na mjomba yangu ilianza kukua!
Ulemavu wangu ulinifundisha kwamba kuwa mwerevu shuleni hakuelezei thamani yako. Maisha yangu bado yana maana. Sisi sote tuna vipawa na talanta tofauti na vinaweza kutumiwa kwa njia nyingi, hivyo yafaa kupanua fikra! Kuwa mlemavu pia hakukufanyi wewe uwe uliyeshindwa. Bado unaweza kufanikisha ndoto zako na kuwa unayetaka kuwa! Ikiwa ninaweza kufanya basi na wewe unaweza!
Share your feedback