Kukabiliana na wanyanyasaji

Nilijifunza kuwa na msimamo

Faridah mwanafunzi mwenzangu alikuwa ananyanyaswa daima. Wasichana wa darasa la juu walimchokoza bila sababu yoyote. Walipitisha jumbe duni, kuweka vitu vilivyonuka kwenye mfuko wake, au kumcheka uwanjani.

Hata ingawa mimi na marafiki zangu tuliona hilo likitendeka na tulitaka kulikomesha, tuliogopa. Hatukutaka kuwa lengo la wasichana hawa duni.

Lakini rafiki yangu mmoja alishiriki nakala kutoka Springster kuhusu kuzungumzia mwenyewe kati yetu, na sote tulihisi kuwa na nguvu sana. Ilinifanya nifikiri kuhusu Faridah, na jinsi anavyoweza kuwa na woga sana kuzungumza. Naamini hakuna mtu yeyote anayestahili kunyanyaswa, najua sio sawa.

Niliwaambia marafiki zangu kuwa wakati mwingine nikiona kundi lile la wasichana duni wakimnyanyasa Faridah, ningemsimamia. Nilikuwa na wasiwasi, lakini nilijua marafiki zangu pia wangeniunga mkono ikiwa jambo lolote lingeenda visivyo. Siku iliyofuata darasani, wasichana wawili wa wale duni walianza kupitisha ujumbe kuhusu Faridah. Wakati ujumbe ule ulinifikia ilinibidi nizungumze, hivyo nilisimama na kwenda mbele ya darasa na nikazungumza na mwalimu wetu:

“Samahani Bi Oku, nimepokea ujumbe ambao sio mzuri sana kuhusu mmoja wa wanafunzi wa darasa. Naamini huu ni unyanyasaji na nadhani sio sawa. Ningependa sana sote tushirikiane ili kusitisha hali hili na tuwe wasaidizi zaidi kwa kila mmoja.”

Bi Okumu alishirikiana na wale wasichana duni pamoja na wazazi wao kuwafunza mbona unyanyasaji sio sawa na inaweza kuwa hatari kwa waadhiriwa. Faridah alishukuru sana, na akaanza kuwa mwenyewe tena. Tangu siku hiyo darasani, Bi Oku aliniomba kuwa mwakilishi wa ‘kupinga unyanyasaji’ shuleni na mara nyingi nizungumze katika hafla za shule ili kushiriki vidokezo vyangu kusaidia kusitisha unyanyasaji.

Ninawaambia wanafunzi jinsi ya kuripoti unyanyasaji kwa mtu mzima aliyeaminika anayeweza kusaidia. Wasijiweke hatarini au kuwa na fujo kwa wanyanyasaji. Waulize marafiki zako wakusaidie kukuunga ili usilazimike kuifanya pekee yako. Na, muhimu zaidi, ujue kwamba una uwezo wa kuisitisha. Inaweza kumchukua tu mtu mmoja kuzungumza kubadilisha maisha ya mtu mwingine – simama leo!

Share your feedback