Ninapenda kila kitu kuhusu magari - uhuru, kasi, maeneo unayoweza kuyaona! Lakini nimewahi tu kuwa abiria na niko tayari kuketi katika kiti cha dereva!
Ninatamani zaidi kupata leseni yangu ili niweze kufanya mazoezi ya kuendesha gari hata zaidi na kujitahidi kufikia ndoto zangu za kuwa dereva mtaalamu wa binafsi.
Moja ya marafiki wa kaka zangu ni dereva na anasema kuwa inafurahisha zaidi kugundua miji mipya na kuzungumza na aina zote za watu.
Ninaposikia hivi, hunifanya nitake kuwa dereva pia lakini ninaogopa kuwalezea wazazi wangu kuwa hiki ndicho ninachotaka kukifanya baadaye.
Nilizungumza na dadangu kuhusu hili na alinipa ushauri bora zaidi.
Aliniambia niwe tayari kwa maswali na wasiwasi walionao. Kama vile nitakavyopata mafuta au gari ambalo ningeweza kufanyia mazoezi.
Alinikumbusha pia kuzungumza nao wakati ambapo wametulia au hawana haraka yoyote. Kwa hiyo nilipanga kuzungumza na wazazi wangu wakati wa wikendi, kwa kuwa ninafahamu kuwa wakati wa siku za wiki huwa wamechoka kutokana na kazi na kumpeleka na kumchukua ndugu yangu mdogo kutoka shuleni.
Ushauri wake wa mwisho ulikuwa kwamba, iwapo wazazi wangu watakosa subira nami, nibaki mtulivu na nisikilize kwa heshima na kujaribu kuelewa mtazamo wao ili niweze kujitahidi kushughulikia masuala yao na kuzungumza nao tena wakati mwingine.
Nilipozungumza nao - mwanzoni babangu alisema kuwa hajafurahishwa na suala langu la kutaka kuwa dereva.
Kwa bahati nzuri, nilikuwa nimejitayarisha zaidi kwa gumzo letu - kwamba alipozua suala lolote, nilikuwa tayari na jibu la kumpa. Kila wakati nilipojibu maswali yake - alianza kukubaliana na wazo langu polepole.
Kwa sababu pia nilikuwa nimefanya mazoezi ya mazungumzo na dadangu mara chache kabla, niliweza kuwa mtulivu na kusikiliza masuala yao vizuri. Kutokana na utulivu wangu, wazazi wangu pia walidumisha utulivu wao.
Niligundua kuwa walitaka tu niwe salama na niwe na mstakabali wa kupendeza! Ninafuraha zaidi nilizungumza nao kuhusu adhma zangu na kupata uungwaji mkono wao kikamilifu.
Share your feedback