Rafiki wangu wa dhati alifuata ndoto zake - na akafanikiwa!

Na sasa ananisaidia kufikia zangu

Kuwa na ndoto kuhusu ni nani na ni nini tunachotaka kuwa kunaweza kutisha kidogo. Lakini punde tu unapojiruhusu kuiota, utashangazwa na unachoweza kutimiza. Rafiki wangu wa dhati Ezra aliamua kufuata ndoto yake, na hakuangalia nyuma. Sasa ananihimza kufuata ndoto zangu pia!

Ezra amekuwa akitaka kuwa mfinyanzi, aliota kuhusu kutengeneza vyombo vya udongo - kuanzia bakuli na vyombo vya maua hadi vinyago mahiri zaidi.

Wazazi wake walimtaka afanye kitu thabiti na kikubwa zaidi, kama vile kuwa daktari au kuwa mwalimu. Alikuwa mwerevu, lakini alikuwa pia mbunifu moyoni na hiyo ndio sababu alitaka kufuatilia anachopenda ambacho kinamwezesha kuwa zote.

Ezra alipenda kuanza na wazo na kutumia mikono yake kuibadilisha kuwa kweli. Alichukua saa nyingi kutengeneza vinyago. Hakuna mtu aliyekuwa na mkono thabiti kama wake, ambayo ilifanya mapambo kwenye kazi yako kuwa nzuri sana. Kuona tabasamu kwenye nyuso za watu alipowaundia kitu kulimfanya afurahi sana.

Alianza kwa kutengeneza vitu vidogo kwa marafiki wake. Alipopata maoni mazuri, aliamua kuanzisha kakibanda kadogo siku za wikendi akiwa bado shuleni.

Sasa anauza kazi zake katika maduka makubwa katika jiji lake. Yeye hutumia mikono yake kutengeneza sanaa yake na anafurahia pia changamoto za kuendesha biashara yake mwenyewe.

Safari ya Ezra ya kutumiza ndoto yake haikuwa rahisi, na haikufanyika mara moja. Lakini alichukua hatua ndogo kila siku ili kuhakikisha anafika hapo.

Hapa kuna baadhi ya mawaidha aliyonipa ambayo unaweza pia kuyafuata!

  • Hakuna ndoto kubwa sanaa, ndogo sana au ya upuzi. Usijinyime ndoto zako mwenyewe. Zimiliki, na ujue unazifaa.
  • Jiruhusu kuziona ndoto zako. Jaribu kuunda ubao wa ndoto. Kata na uunganishe picha zinazokuhimiza - watu, maeneo, na kazi. Ziweke mahali unapoweza kuziona unapoamka au katika jarida lako la kibinafsi. Kwa njia hiyo, utaweza kuona ndoto yako kila siku.
  • Shiriki ndoto zako na wengine. Itasaidia kuzifuatilia, na itaunda pia mifumo ya usaidizi karibu na wewe. Hujui ni nani anayeweza kukusaidia njiani kufikia ndoto zako.

Kwa hivyo ni nini kinachokuzuia? Anza sasa!

Share your feedback