Ndugu yangu hupenda kumsaidia mama jikoni - ana hisia nzuri zaidi za ladha! Atamsaidia katika kuchagua mboga nzuri zaidi sokoni na hata ameanza kupanda bustani yake mwenyewe ya mboga na nyanya kwenye uwanja wa nyuma ya nyumba yetu.
Mimi huonekana kuunguza chochote ambacho hujaribu kupika. Lakini nina uraibu wangu - kumsaidia babangu kurekebisha magari. Babangu ni mekanika na tangu nilipokuwa msichana mdogo, nilipendelea kuwa msaidizi wake. Kwa kawaida ningembebea tu vitu na kutazama, lakini siku za hivi karibuni ameniruhusu kufanya kazi za maana.
Biashara yake inakua na anahitaji usaidizi rasmi. Ninaenda kutuma ombi la jukumu la kuwa msaidizi wake, lakini marafiki zangu na familia yetu pana inaona kuwa ni kaka yangu anayepaswa kuwa akifanya kazi na babangu.
Kaka yangu hataki kuwa mahali popote karibu na magari chafu au harufu - anapendelea kuwa nje katika ulimwengu kwenye bustani akitazama vitu vinapokua. Anatumia muda wake wa majira ya kiangazi kama mpishi mdogo katika mkahawa wa eneo - kwa hiyo hana muda wa magari.
Hamna njia yoyote ambapo ningeruhusu maoni ya watu kunizuia kufanya kazi hiyo - Nilijua kuwa nina ujuzi kwa kuwa nilikuwa nimelelewa kwenye gereji hiyo ya magari. Kwa hiyo nilitafuta kauli ya kazi ya kumshawishi babangu kuwa ninafaa.
Nilimwambia kuwa angenichukulia kama mfanyakazi mwingine yeyote na anipe jaribio la kazi na iwapo nitafaulu - ninapaswa kupata kazi. Alinipa majaribio kwenye gari kama vile kubadilisha nyembe za kifutio cha kioo na kupaka rangi iliyobanduka. Nilipata matokeo mazuri zaidi!
Marafiki zangu ambao mwanzo walicheka nilipowaambia kuwa nilitaka kazi, kwa sasa wamefurahishwa zaidi na kazi yangu.
Ninafuraha zaidi kuwa mimi na kaka yangu tulifuata ndoto zetu na hatukusikiliza maoni ya watu wengine kuhusu kitu ambacho tunapaswa kufanya.
Share your feedback