Mwaka wa kwanza kama mamake Ruthie

Nimeitikia changamoto!

Kuwa mama Ruthie ndilo jambo nzuri sana kuwahi kunitendetekea. Lakini ina changamoto zake. Ni poa sababu kila wakati nikifika nyumbani kutoka shule ya uhasibu, yeye anakimbia nyuma ya pazia, kisha ananiambia kwa sauti nimtafute. Inafurahisha sana, sababu huwa tayari naiona miguu yake midogo. Sikuwa nadhani itakuwa hivi, lakini siku hizi huwa nakimbia nyumbani ili kuona miguu yake midogo nyuma ya pazia.

Nilipogundua nilikuwa mjamzito nikiwa na miaka 16, niliingiwa na wasiwasi na sikujua lipi lingenitokea siku za mbeleni. Bahati nzuri Mama alinitia moyo niwe mama mzuri na kufuatilia ndoto zangu.

Mama, Ruthie na Nathan ambaye ni jirani wetu ndio watu wa muhimu zaidi katika maisha yangu. Sidhani ningekuwa hapa bila wao. Nakumbuka nilipotoka hospitali na Ruthie baada ya kujifungua ilikuwa ngumu kiasi katika wiki za mwanzo, lakini Mama alisema tungepata suluhisho.

Mama alimwomba Nathan aniongeleshe kuhusu kusomea uhasibu. Daima nimekuwa mzuri sana na hesabu shuleni. Mwaka jana, kabla ya kumpata Ruthie, nilituzwa kwa kuwa mwanafunzi bora katika somo la hisabati darasani kwangu. Nathan ni mwalimu shuleni na alisema nina talanta. Nashukuru kuwa alisema maneno yale, sababu baada ya kumpata Ruthie, nilihisi kuchanganyikiwa. Lakini cha kushangaza ni kuwa, nitahitimu miezi 6 ijayo na nimejawa na hamu!

Natamani siku moja kufanya kama mhasibu! Nilisoma kwenye intaneti kuwa itabidi nisome kwa bidii ili nipate diploma, na nitakapohitimu nitafanya kazi kama mhasibu. Pengine hata siku moja nitafungua kampuni yangu ya uhasibu!

Nimesoma mengi mwaka jana. Nikagundua kuwa naweza, mimi ni mama mzuri kwa Ruthie, na naweza kufanya chochote ikiwa nitajiamini.

Share your feedback