Lakini ninataka tu niwe mimi!
Wazazi wangu wananisumbua kila wakati kuhusu jambo fulani. Kama, jinsi ninavyopenda kuvaa tisheti nzee na ninafurahi kuvaa suruali ndefu, lakini mama yangu husema wasichana wanapaswa kuvaa sketi pekee na marinda marefu. Pia yeye husema kwamba ninatumia simu yangu sana. Ninahisi kwamba siwezi pata raha tena.
Baba pia amekuwa mkali kwangu. Ninapenda kushughulika komputya na kuandika codes, lakini anachukia wazo langu kufanya kazi katika sayansi ya komputya. Alinifanya niwache somo lile mwaka huu.
Ndugu yangu anaweza kula, kuvaa na kufanya anachotaka. Hili linanikasirisha sana.
Hivi majuzi mama yangu pia ameanza kukosoa marafiki zangu, akisema anafikiri sio werevu vya kutosha.
Ninapenda marafiki zangu, wao hunisaidia na uchu na ndoto zangu. Mama anafikiria wao ni wa kunipotosha fikra na baba anasema msichana hafai kuwa rafiki na wavulana katika umri wangu, kwani watu watanifikiria visivyo. Ninafikiri haya yamezidi. Marafiki zangu hunicheka kwa sababu wazazi wangu ni wakali.
Ni sherehe ya kuzaliwa ya rafiki wangu wa dhati Abila wikendi hii na wazazi wangu wamesema siwezi kwenda. Hawanipi sababu mbona nisiende.
Ninawaheshimu wazazi wangu na ninajua wananitunza tu, lakini pia ninataka kuwa na usemi zaidi katika maamuzi yanayonihusu. Ninafikiri nimethibitisha kuwa ninaweza kuaminika, kwa hivyo natumai wanaweza kuwa wazi kwa mazungumzo nami.
Nilichukua muda nitulie na nikahakikisha kwamba nitazungumza nao kama sijakasirika. Nilipokuwa tayari, niliwaambia kwamba ninajivunia mwanamke niliyekuwa. Kwamba ninasoma kwa bidii na ninathamini mahusiano yangu ya urafiki – na kwamba ningependa msaada wao.
Niliwapa nafasi na muda wa kueleza wasiwasi wao na waliheshimu hoja zangu pia. Mwishoni mwa mazungumzo, wazazi wangu kwa pamoja walivutiwa na jinsi nilivyokomaa. Kwa pamoja walikubali kwamba wangenisaidia katika maamuzi yangu. Mama hata ameahidi kuwacha kuninunulia marinda makubwa!
Share your feedback